• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 10:06 AM
Sonko aonyesha kamera za CCTV zilizosheheni kwake akisema wezi kufikia pesa zake ni ndoto

Sonko aonyesha kamera za CCTV zilizosheheni kwake akisema wezi kufikia pesa zake ni ndoto

Na WAANDISHI WETU
ALIYEKUWA gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amekanusha madai kwamba wezi wanaweza vamia nyumbani kwake na kumuibia kitita cha pesa alichoonyesha mtandaoni.

Kwenye video aliyopakia TikTok, Sonko alionyesha kamera za siri za CCTV akisema kuwa ni vigumu sana mwizi kuingia nyumbani kwake bila kuonekana.

Akipuuzilia madai kwamba ataporwa akiwa amelala, Sonko alisema kuwa nyumbani kwake huwezi ingia.

“Ukiruka hivi tunakuona. Ile mizinga iko huku…Utaingilia wapi hapa na tunakuona kila mahali,” akasema akionyesha kamera za CCTV zilizoko kwake.

Sonko alivuma wiki jana baada ya kuonyesha pesa alizokuwa nazo nyumbani kwake.

Mwanasiasa huyo aliyekuwa akimjibu mwanafamilia aliyemkwaza kwa matusi, alionyesha pesa zilizokuwa kwa noti za dola na elfu huku akikanusha madai kuwa yeye ni maskini.
Kwenye video hiyo, Sonko alionyesha makasha aliyodai yamejaa pesa kabla ya kufungua moja kuthibitisha kwamba hajafilisika.

Akionekana kutojali sheria inayozuia watu kuweka mamilioni ya pesa ndani ya nyumba zao kwa sababu za kiusalama, Sonko aliongea kwa hasira akimshutumu mwanafamilia huyo ambaye hakumtaja jina.
“Eti unasema sina pesa kwa sababu sisaidii watoto. Nani alikwambia mtu aliye na zaidi ya miaka 18 ni mtoto. Mtu ambaye amejifungua, ambaye amesomeshwa hadi akamaliza shule. Niko na pesa, lakini sio za kutumia kwa watoto. Niko na pesa za kutumia na wake zangu,” akasema huku akiachilia msururu wa matusi.

Wakenya wengine haswa watu tajika walichukulia video hiyo na wao pia wakaanza kuringisha pesa walizo nazo.

  • Tags

You can share this post!

Magavana walia serikali yaua ugatuzi

Rai Serikali ihifadhi vyumba vya mateso Nyayo kama...

T L