• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:30 PM
Stephen Letoo apamba siku maalum ya kuzaliwa kwa Chemutai Goin   

Stephen Letoo apamba siku maalum ya kuzaliwa kwa Chemutai Goin  

NA MERCY KOSKEI

MWANAHABARI wa masuala ya kisiasa wa runinga ya Citizen, Stephen Letoo alimwandalia mtangazaji mwenzake Chemutai Goin sherehe ya kukata na shoka kuadhimisha siku maalum ya kuzaliwa kwake.

Bw Letoo alimpeleka Chemutai kwenye hoteli moja maarufu Ngong Road, Kaunti ya Kajiado ili kusherehekea siku yake maalum kuingia duniani, pamoja na marafiki.

Mama huyo wa watoto wawili alivali rinda jeupe wakati wa sherehe hiyo.

Katika video iliyosambazwa na Letoo kwenye mitandao ya kijamii, Oktoba 1, 2023, Bi Chemutai alionekana akicheza muziki, wenzake wakimmiminia pesa huku marafiki zake wakishangilia.

Letoo alimzunguka, huku ‘akimbandika’ noti za pesa kwenye mavazi.

“Inapofika siku maalum kukumbuka kuzaliwa kwa Jane Chemutai Goin, kila kitu kinasimama…! Tunazima. Heri ya kuzaliwa NyarLessos,” Letoo aliskika akimpongeza, kupitia video ambayo pia alipakia kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook.

Letoo na Chemutai si wafanyakazi tu bali ni marafiki wa karibu.

Mwaka jana, 2022, Letoo aliwashangaza mashabiki mitandaoni baada ya kumzawadi Chemutai siku yake ya kuzaliwa.

Letoo alimsherehekea Goin kwa njia ya pekee.

Wawili hao ni maripota guru wa masuala ya kisiasa Citizen TV, runinga inayomilikiwa na Shirika la Royal Media Services (RMS).

 

  • Tags

You can share this post!

Kibra itakuwa sawa na mtaa wa kifahari wa Karen, Ruto aahidi

Sherehe ya ‘Sapanaa’ kutawaza viongozi katika jamii ya...

T L