• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
TEKNOLOJIA: Sifa za kipekee za simu aina ya Tecno Phantom X2

TEKNOLOJIA: Sifa za kipekee za simu aina ya Tecno Phantom X2

NA WINNIE ONYANDO

MNAMO Januari 17, 2023, kampuni ya kutengeneza simu ya Tecno ilizindua simu mpya aina ya Phantom X2 inayolenga wasanii.

Simu hiyo ina sifa za kipekee inayoifanya kuwa na utendakazi bora.

Simu hiyo mpya inajumuisha Phantom X2 Pro 5G na Phantom X2 5G.

Baadhi ya sifa hizo ni:

Muundo

Tecno Phantom X2 una jalada la nyuma lililotengenezwa na vifaa maalum ili kulinda mazingira.

Simu hiyo ina jalada lenye rangi ya machungwa.

Kamera

Kila mtu anapenda simu iliyo na kamera nzuri na kwa kutumia simu hiyo ya Tecno Phantom X2, unauhakika utapacha picha nzuri.

Phantom X2 Pro 5G ndiyo simu mahiri ya kwanza duniani kuwa na lensi (lenses) ya picha nzuri.

Lensi ina tundu la F/1.49.

Ikijumlishwa na urefu wa 65mm, lensi ya picha ya 2.5x inaweza kutengezwa na kuonekana kama ya megapixel 50.

Hii huwapa watumiaji uwezo wa kunasa picha nzuri na wima zinazolingana na picha za kitaalamu.

Utendakazi

Hakuna anayependa simu inayojikokota.

Simu ya Phantom X2 ina MediaTek Dimensity 9000, ambayo ni 4nm octa-core processor iliyooanishwa na nafasi ya 12GB RAM ya LPDDR5X (inayoweza kupanuliwa hadi 15GB) na 256GB.

Kwa kutumia aina hii ya simu, mtumiaji anaweza kupakua Apu kadhaa kwenye simu yake bila kujali uwezo wa utendakazi wake.

Uwezo wa betri

Tecno Phantom X2 ina betri ya 5160mAh.

Ukiwa na aina hii ya simu, huna presha ya simu yako kuisha moto.

Bei na upatikanaji

Simu hizo zinapatikana katika maduka rasmi ya Tecno kwenye mtandao wa kijamii ya Jumia, Safaricom PLC, tovuti ya Tecno na maduka ya reja reja ya Tecno.

Bei yake ni kati ya Sh67,999 (Phantom X2) na Sh82,999 (Phantom X2 Pro).

  • Tags

You can share this post!

Achani sasa roho mkononi mahakama ikiamua ushindi wake

Magoha alijua siku ya mauti imewadia

T L