• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:50 AM
UJASIRIAMALI: Jinsi Shiru Ndirangu anavyopiga hatua kwa kuuza matunda na mboga nje ya nchi

UJASIRIAMALI: Jinsi Shiru Ndirangu anavyopiga hatua kwa kuuza matunda na mboga nje ya nchi

Na MAGDALENE WANJA

NDOTO ya Shiru Ndirangu tangu utotoni ilikuwa ni awe rubani ila hakupata nafasi ya kusomea kazi hiyo baada ya kukamilisha Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne.

Badala yake alisomea kozi ya Biashara, Usimamizi na Masuala ya Kifedha katika Chuo Kikuu cha Strathmore.

“Nilipendezwa sana na kazi ya urubani kwani nilitaka kusafiri kote ulimwenguni na kujionea mazingira tofauti, ila niligundua baadaye kuwa sikuhitaji kuwa rubani ili kujionea ulimwengu,” anasema Shiru.

Zama hizo za elimu ya chuoni, alitumia muda wake wa mapumziko katika shamba la wazazi wake ambapo walikuza aina mbalimbali za matunda na mboga.

Bi Shiru Ndirangu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrex Gold Limited. PICHA | MAGDALENE WANJA

Wakati huo, hakujua alichotaka kufanya baada ya kukamilisha masomo yake, japokuwa alipendezwa sana na kazi ambayo wazazi wake walikuwa wakifanya.

Alipofuzu mnamo mwaka 2008, aliajiriwa katika benki moja hapa nchini.

“Nilifanya kazi hiyo kwa muda mfupi sana na nikaamua kuacha kazi hiyo kusudi niwasaidie wazazi wangu katika kilimobiashara,” anasema Shiru.

Kwa sasa, Shiru ni  Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Afrex Gold Limited ambayo hupakia matunda na mboga na kuuza katika nchi mbalimbali. Matunda wanayouza nje kwa idadi kubwa ni maparachichi.

Bi Shiru Ndirangu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrex Gold Limited. PICHA | MAGDALENE WANJA

Kazi yake kama Mkurugenzi Mkuu ni kutoa mwongozo na kuhakikisha kuwa kampuni inafikia malengo yake.

“Kwa sasa tunatekeleza mradi utakaowasaidia wakulima wadogowadogo kuongeza mapato na kuhakikisha kuwa mapato hayo yanafikia ubora na kiwango kinachotakikana,” anadokeza.

Chini ya mradi huo, wanalenga kuhakikisha kwamba angalau wamepanda miti zaidi ya 80,000 ya kuzaa maparachichi.

  • Tags

You can share this post!

Ajitahidi kuwakwamua wanawake kiuchumi katika mitaa ya...

Mung’aro ang’ara mahakamani

T L