• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
UJAUZITO NA UZAZI: Uvimbe ndani ya pua ya mtoto

UJAUZITO NA UZAZI: Uvimbe ndani ya pua ya mtoto

NA PAULINE ONGAJI

SHIDA ya uvimbe kujitokeza katika sehemu ya ndani ya pua la mtoto husababishia wazazi wengi wasiwasi.

Hali hii inayotambulika kama Nasal Polyps kwa lugha ya kitalamu, huhusisha kuvimba kwa njia ya pua na kwenye mianzi ya pua kwa zaidi ya wiki 12.

Uvimbe huu huwa mwepesi na hausabaishi maumivu, na hivyo ikiwa uvimbe ni mdogo sio rahisi kuutambua. Zikiwa nyingi au kubwa zaweza ziba mianzi ya pua.Mbali na watoto, hali hii pia huwakumba watu wenye umri wa makamo, lakini shida huisha baada ya matibabu. Hata hivyo, ni kawaida kwa uvimbe huu kujitokeza tena hata baada ya kutibiwa.?Ishara za uwepo kwa uvimbe puani

Kutokwa na kamasi kila mara Pua kuziba kwa muda mrefu Kukohoa na kukumbwa na matatizo unapomeza chakula Kutokuwa na hisia za kunusa au ladha Kuumwa na kichwa Uchungu kwenye meno Kukoroma unapolala Mwasho kwenye macho

Unatakiwa kumwona daktari ikiwa dalili hizi zitaendelea kwa zaidi ya siku kumi.

Kumbuka kuwa ishara hizi ni sawa na za mafua.

Aidha, unashauriwa kutafuta usaidizi wa kimatibabu endapo utashuhudia dalili zifuatazo:

  • Ugumu unapopumua
  • Dalili zilizotajwa zinapozidi
  • Unapokumbwa na ugumu wa kuona vizuri au matatizo unapopindua macho.
  • Unapokumbwa na uvimbe katika sehemu ya macho
  • Kichwa kinapozidi kuuma maumivu haya yakiambatana na homa au ugumu wa kusongesha kichwa.

Ni nini kinachosababisha hali hii? Ingawa kuna tafiti kadhaa kuhusu nasal polyps, wanasayansi hawajafanikiwa kupata sababu halisi zinazochochea hali hii.

Matibabu tofauti hutumika kutibu hali hii lakini hutegemea na kiwango cha uvimbe. Matibabu huangazia sana jinsi ya kupunguza saizi ya uvimbe ili kukabiliana na ishara.

  • Tags

You can share this post!

HUKU USWAHILINI: Kuna jibaba huku limeshindwa kumdekeza mke...

Wito waziri Machogu aruhusu wanafunzi kupata muda mwingi wa...

T L