• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
ULIMBWENDE: Ili usiwe na chunusi, epuka vyakula hivi

ULIMBWENDE: Ili usiwe na chunusi, epuka vyakula hivi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

VYAKULA fulani vinaweza kuchangia chunusi kwa kusababisha kutokea kwa uvimbe au kuchochea homoni maalum zinazoathiri ukuaji wa chunusi.

Chunusi ni hali ya kawaida ya ngozi inayoathiri watu wengi duniani.

Visababishi vya chunusi ni vingi ikiwemo uwepo wa sebamu na keratini, bakteria wanaosababisha chunusi. Pia homoni, vinyweleo vilivyoziba, na uvimbe ni sababu nyingine za chunusi kutokea.

Uhusiano kati ya lishe na chunusi umekuwa na utata, lakini tafiti nyingi zinaonyesha kuwa lishe inaweza kuwa na jukumu kubwa katika ukuzaji wa chunusi.

Nafaka iliyosafishwa na sukari

Watu wenye chunusi huwa wanatumia wanga au kabohaidreti iliyosafishwa zaidi kuliko watu walio na chunusi kidogo au wasio na chunusi.

Vyakula vyenye wanga au kabohaidreti iliyosafishwa ni pamoja na mkate, nafaka, au kitindamlo kilichotengenezwa kwa unga mweupe.

Kwenye orodha hiyo pia kuna pasta iliyotengenezwa na unga mweupe, wali mweupe na tambi, lakini pia soda na vinywaji vingine vyenye sukari.

Matumizi ya mara kwa mara ya vyakula vyenye sukari au mafuta mengi yanahusishwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na chunusi na kuongezeka kwa sukari ya damu.

Kabohaidreti iliyosafishwa huingia haraka ndani ya damu, hali ambayo huongeza kasi ya viwango vya sukari ya damu.

Wakati sukari ya damu inapopanda, viwango vya insulini pia hupanda kusaidia kuhamisha sukari ya damu kutoka kwa damu na kuingia kwenye seli zako.

Bidhaa za maziwa

Vijana ambao wanatumia maziwa au aiskrimu mara kwa mara wana uwezekano mkubwa wa kuwa na chunusi.

Bidhaa za maziwa zinaweza kuongeza viwango vya insulini na kuzua hali ambayo inaweza kuzidisha ukuaji wa chunusi. Maziwa ya ng’ombe pia yana asidi ya amino ambayo huchochea ini kutoa insulin fulani zaidi, ambayo inahusishwa na ukuzaji wa chunusi.

‘Fastfood’

Vyakula vilivyopikwa au kutayarishwa kwa mafuta mengi. PICHA | MARGARET MAINA

Chunusi zinahusishwa sana na kula chakula chenye kalori nyingi, mafuta, na kabohaidreti iliyosafishwa.

Vyakula vya haraka vinaweza kuongeza hatari ya chunusi.

Kula vyakula vya kukaanga kwa mafuta mengi mara kwa mara kunaongeza hatari kwa asilimia kubwa.

Vyakula vya haraka vinaweza kuathiri usemi wa jeni na kubadilisha viwango vya homoni kwa njia ambayo inakuza ukuaji wa chunusi.

Vyakula vinavyokupa mzio

Chunusi zinachukuliwa kuwa ni ugonjwa unaotokana na vichocheo fulani ikiwa ni pamoja na kile kinachoweza kusababisha ‘allergy’ au mzio. Mwili ukitambua uwepo wa chakula cha mzio, molekuli fulani hotolewa na zinazozunguka mwilini. Hizi zinaweza kuzidisha chunusi kwa kiwango fulani.

MUHTASARI

Kula chakula chenye asidi ya mafuta ya Omega-3, probiotiki, chai ya kijani, matunda, na mboga kunaweza kuwa njia bora ya kujikinga dhidi ya ukuaji wa chunusi. Vitamini A, D, na E, pamoja na zinki, zinaweza pia kusaidia kuzuia chunusi.

  • Tags

You can share this post!

Hii imeoza

Mwanafunzi aliyemuua mwenzake kwa kisu akamatwa Lamu

T L