• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Vituko: Sonko athibitisha ‘blingi’ zake si feki

Vituko: Sonko athibitisha ‘blingi’ zake si feki

Na MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA gavana wa Nairobi Mike Sonko alithibitisha kuwa blingi (vito) anavyovaa vya dhahabu si ghushi.

Kwenye video aliyoposti mtandaoni, Sonko alimsuta mwakilishi wa wadi ya Kileleshwa Robert Alai kwa kueneza uvumi kuwa vito vyake ni feki.

Alai na Sonko wamekuwa wakivutana mtandaoni kuhusu uhalali wa vito anavyovaa Sonko huku wakisutana kwa maneno yenye matusi.

“Wakati mwingine ni vyema kumuonyesha anayekuchukia kama mwakilishi mmoja wa wadi na wenzake kuwa wamekosa haswa wanapojihusisha na mambo wasiyojua ukweli wake. Rafiki yangu Roba, niliwaendea wauzaji vito wawili na wakakagua iwapo vito vyangu ni feki kama ulivyodai,” akaandika.

Kisha akaendelea, “Tazama video hii kwa makini na utagundua iwapo ulikuwa unasema ya kweli au la. Hata hivyo, unaweza mtafuta muuza vito wako mwenyewe na nitasalimisha vito vyangu vipimwe. Iwapo vitakuwa feki ofa yangu ya kumjengea nyanya yako nyumba kijijini bado ipo.”

Mchakato wa iwapo vito anavyovaa ni feki au la ulianzia wakati Alai alidai kuwa vito anavyovaa Sonko havifiki thamanI ya Sh20, 000.

Aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, “Feki. Hivyo vitu alivyovaa haviwezi kuwa hata Sh20, 000. Thamani yake ni chini zaidi. Rangi ni ya dhahabu lakini vitu vyenyewe feki.”

 

  • Tags

You can share this post!

Madaraka Dei 2023: Rangi maridadi za vikosi vya pamoja vya...

Utata wa kesi ya mvulana wa miaka 13 akinajisi msichana wa...

T L