• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Viva, Miguna Miguna amsuta Rais Museveni kwa pendekezo kujinunulia nguo za Sh350 milioni, Uganda ikizongwa na umaskini  

Viva, Miguna Miguna amsuta Rais Museveni kwa pendekezo kujinunulia nguo za Sh350 milioni, Uganda ikizongwa na umaskini  

Na WANGU KANURI

WAKILI Miguna Miguna amemkemea Rais wa Uganda Yoweri Museveni kufuatia pendekezo la bajeti ya Sh350 milioni kujinunulia nguo, viatu na malazi mapya.

Miguna aliyesema kuwa bajeti hiyo ni jambo la kuonewa haya haswa katika bara la Afrika, aliuliza ni vipi rais huyo ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 37 hana nguo za kutosha.

Kwenye ujumbe wake mtandaoni, Miguna alikosoa rais Museveni akisema kuwa atajiaibisha sana kupitia pendekezo hilo.

“Hata baada ya kuwa kwenye mamlaka kwa miaka 37 unataka kuniambia Museveni hana suti za kutosha? Hii ni aibu kwa Afrika,” akaandika.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, viongozi wa upinzani nchini humo wamekemea sana pendekezo hilo la bajeti wakisema kuwa inapaswa kupunguzwa.

Hata hivyo, bajeti hiyo ilikuwa vivyo hivyo miaka ya awali.

Mbunge Ibrahim Ssemujju Nganda akiwa mmoja wa wabunge waliokataa bajeti hiyo alisema, “Kuna milioni 350 za kumnunulia rais Museveni nguo na bajeti hiyo ilikuwa mwaka jana. Hii ina maana kuwa nchi inatumia Sh36, 000 kila siku kwa nguo za rais.”

Akaongezea, “Rais wetu si staa kutoka Hollywood ndiposa abadilishiwe nguo zake kila siku. Yeye ni rais wa nchi yenye umasikini mkubwa. Mbona tumnunulie nguo za milioni 350 kila mwaka? Nguo za mwaka jana zilienda wapi?”

Isitoshe, Ssemujju aliuliza, “Tunawezaje kuwa tunatumia milioni moja kwa hafla wakati barabara katika mji mkuu hazipitiki? Pesa hiyo inayotumika kwenye hafla hizo inapaswa kukarabati barabara za Kampala na Wakiso.”

 

  • Tags

You can share this post!

Njugush na Wakavinye wafunguka kuhusu kufanya kazi pamoja...

Anavyovuna katika biashara ya kuchoma nyama  

T L