• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 10:00 AM
Waziri Kindiki: Serikali ilichelewa sana kufika Shakahola    

Waziri Kindiki: Serikali ilichelewa sana kufika Shakahola   

 

Na WANGU KANURI

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki alijutia serikali ilichelewa kufika Shakahola kabla maisha ya wengi hayajapotezwa.

Akizungumza Jumapili, Juni 4, 2023 Kindiki alisema kuwa wakati serikali ilikuwa inaangazia matukio ya Shakahola, mwanamume mmoja alikuwa ameua watu wengi kuliko wale waliwahi uliwa na magaidi miaka 10 iliyopita.

Akisisitiza kuwa serikali imeweka mikakati kudhibiti makanisa kisheria, Profesa Kindiki alisema kuwa baadaye Wakenya watahusishwa kuafikia na kukarabati mikakati hiyo.

Isitoshe, aliwaomba kujitokeza kwa wingi na kuhusika katika mjadala huo ili kuzuia visa kama vya Shakahola.

“Kama serikali tunajutia sana kuitika mwito wa mauaji ya Shakahola baada ya muda. Hata hivyo, serikali imejitahidi kuwakamata na kuwaondoa wahubiri na viongozi wanaotumia mambo ya kiroho kuwalaghai wafuasi wake.”

Mhubiri tata Paul Mackenzie anahusishwa na mauaji ya halaiki ya wafuasi kule Shakahola kupitia dini zenye mafunzo potovu.

Zaidi ya miili ya washirika 200 wa Good News International Church, kanisa linalomilikiwa na Pasta Mackenzie, imefukuliwa huku ufukuaji ukitarajiwa kuendelea Jumatatu Juni 5, 2023.

Waziri Kindiki alisema makaburi 22 zaidi yanalengwa.

Wengine 613 bado wanasakwa huku mili mingine iliyofukuliwa ikiwa imeoza zaidi kiasi cha maafisa kutojua jinsia yake.

Pasta tata huyo analaumiwa kuhadaa wafuasi wake kufunga bila kula wala kunywa maji, akiwaahidi hatua hiyo itawafanikisha kuonana na Yesu.

  • Tags

You can share this post!

Maisha yamenipiga chenga, Baha akiri akigeukia wafuasi wake...

Mishi Dorah atoka soko, si ‘singo’ tena

T L