• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:50 AM
Zifahamu baadhi ya faida za upupu (stinging nettle)

Zifahamu baadhi ya faida za upupu (stinging nettle)

NA MARGARET MAINA

[email protected]

UPUPU almaarufu stinging nettle, umekuwa ukitumika kama dawa ya mitishamba tangu zama za kale.

Wamisri tangu azali waliitumia upupu kutibu ugonjwa wa yabisi na maumivu ya kiuno, huku wanajeshi wa Kirumi nao wakijisugua upupu ili kusaidia kuwapa joto.

Majani yake yana muundo unaofanana na nywele. Majani haya huuma na pia huwasha athari ikiwa ni kusababisha uwekundu na uvimbe.

Upupu huwa na virutubisho vingi

Majani na mizizi ya upupu hutoa aina mbalimbali za virutubisho, ikiwa ni pamoja na;

Vitamini

Vitamini A, C na K, pamoja na vitamini B kadhaa.

Madini

Kalsiamu, chuma, magnesiamu, fosforasi, potasiamu na sodiamu

Asidi zote muhimu za amino.

Upupu husaidia kupunguza kuvimba

Kuvimba ni njia ya mwili wako kujiponya na kupigana na maambukizo.

Ingawa hivyo, kuvimba kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara makubwa. Upupu au baadhi ya krimu za upupu au bidhaa za upupu zinaonekana kupunguza hali hii pamoja na kupambana na ugonjwa wa yabisi.

Inaweza kupunguza shinikizo la damu

Shinikizo la damu ni hatari kubwa kiafya kwa sababu humweka mgonjwa katika hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi, ambayo ni kati ya sababu kuu za vifo ulimwenguni. Upupu ulitumika jadi kutibu shinikizo la damu.

Ngozi na nywele

Chai ya upupu imethibitishwa inafanya kazi muhimu na ambayo ni kusaidia kusafisha chunusi na ukurutu, na pia kuchochea nywele kung’aa bila kusahau ukuaji mpya wa nywele.

Aidha inaboresha mzunguko wa damu kwenye ngozi, hali ambayo inakuza ukuaji wa nywele.

Hulinda afya ya moyo

Chai ya upupu inaweza kusaidia kulinda mja dhidi ya magonjwa ya moyo na mishipa, kama vile kuganda kwa damu na shinikizo la damu.

Wanywaji wa chai hii wanaweza kupunguza shinikizo la damu. Pia husaidia kupunguza uvimbe kwenye mishipa ya damu, na kuzuia ugonjwa wa moyo.

Afya ya figo na kibofu

Upupu ni diuretiki bora na inaweza kupunguza hatari ya mawe kwenye figo na kibofu cha mkojo.

Zaidi ya hayo, husaidia kuondoa vitu vyenye madhara, ikiwa ni pamoja na taka na sumu kwa haraka na kulinda dhidi ya maambukizi ya kibofu.

  • Tags

You can share this post!

LISHE: Umuhimu wa tunda la kantalupu

MAPISHI KIKWETU: Nyama ya kuku choma iliyoandaliwa kwa...

T L