Habari Mseto

Makanisa yazimwa kuandaa kesha ya Krismasi

December 20th, 2020 1 min read

Na George Odiwuor na Wycliff Kipsang

Serikali imetangaza hatua kali za kuzuia msambao wa virusi vya corona msimu wa sherehe za krisimasi ikiwa ni pamoja na kukataza kesha makanisani.

Kamishna wa Kaunti ya Homa Bay Moses Lilan, alisema ofisi yake imeweka mwongozo mpya kukinga wakazi wasiambukizwe virusi hivyo wanaposherehekea Krisimasi na Mwaka Mpya.

Miongoni wa hatua hizo ni kuwaita maafisa wote wa polisi ambao wako likizoni ili kushika doria kuhakikisha kanuni za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo zitazingatiwa.

Vituo vya magari katika miji mikubwa kaunti ya Homa Bay, huwa na shughuli nyingi watu wakisafiri kutoka Nairobi, Mombasa na miji mingine kuungana na familia zao mashambani.

Bw Lilan alisema kwamba kamati ya usalama ya kaunti na ile ya kukabiliana na corona imeagiza maafisa wa polisi kutoruhusu mikutano yoyote inayoweza kuweka wakazi katika hatari ya kuambukizwa corona

.Alisema hakuna mtu atakayeruhusiwa kuwa nje usiku.