Makarios na DN Hotstars zatiga robo fainali Dennis Oliech Cup

Makarios na DN Hotstars zatiga robo fainali Dennis Oliech Cup

Na JOHN KIMWERE
MAKARIOS 111 (Riruta United) na DN Hotstars FC kila moja imejikatia tiketi ya kushiriki robo fainali za mashindano ya Dennis Oliech Cup baada ya kushinda mechi za hatua ya 16 bora uwanjani NCC Ngong Road, Nairobi.
Makarios ya kocha, Geoffrey ‘Jombe’ Osoro ilitandika Ping FC mabao 2-0 nao wanasoka wa DN Hotstars waliandika ushindi wa magoli 3-0 mbele ya Ngong 1960 FC.Makario ambayo hushiriki mechi za Nairobi West Regional League ilipoteza dakika kumi za kwanza kabla ya kujipanga na kuanza kushusha soka la kuvutia.
Kikosi hicho kilitesa wapinzani wao na kupata bao la kwanza dakika ya 16 kupitia Javan Mukoya. Pande zote ziliendelea kukabiliana ambapo kabla ya dakika 45 kukatika Peter Njenga alifungia Makarios bao la pili.
”Tunashukuru wachezaji wetu kwa ufanisi huo ambapo tunatarajia kufahamu wapinzani wetu katika robo fainali mnamo Jumatatu kati ya FIFA Best na Soka Talent,” katibu wa Makarios, Josphat Karuri alisema.
Nayo Ngong 1960 ilijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kutimiza azma ya kusonga mbele mikononi mwa DN Hotstars.  Washindi hao walivuna mabao hayo kupitia Esau Opiyo, Newton Ochieng na Collins Chibole waliotikisa wavu mara moja kila mmoja.

 

  • Tags

You can share this post!

Kivumbi kikali kushushwa kwenye mechi za BNSL

Talaka ya NASA yakamilika sasa chama cha ODM kikijiondoa