Makipa Ederson na Alisson wa Man-City na Liverpool mtawalia wagawana tuzo ya Kipa Bora wa EPL msimu 2021-22

Makipa Ederson na Alisson wa Man-City na Liverpool mtawalia wagawana tuzo ya Kipa Bora wa EPL msimu 2021-22

Na MASHIRIKA

KIPA Ederson Moraes wa Man-City na Alisson Becker wa Liverpool waligawana tuzo ya Kipa Bora almaarufu Golden Glove baada ya kila mmoja wao kukamilisha msimu kwa kutofungwa bao katika jumla ya mechi 20.

Moraes angali na mkataba wa kuhudumu ugani Etihad hadi 2016. Kipa huyo raia wa Brazil alisajiliwa na Man-City mnamo 2017 na amesaidia miamba hao kutia kapuni mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Tangu aingie katika sajili rasmi ya Man-City kutoka Benfica miaka mitano iliyopita, Ederson amenyanyua pia Kombe la FA na mataji matano ya League Cup.

Kwa upande wake, Alisson alijiunga na Liverpool mnamo 2018 kwa mkataba wa miaka sita baada ya kuagana na AS Roma ya Italia kwa kima cha Sh9.3 bilioni. Fedha hizo zilimfanya kuwa kipa ghali zaidi duniani wakati huo. Tangu wakati huo, amesaidia Liverpool kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), Carabao Cup, Kombe la FA na ubingwa wa EPL.

Liverpool walilemazwa na majeraha katika kampeni za 2020-21 na wakashindwa kuhifadhi ubingwa wa EPL. Hata hivyo, walizoa Kombe la FA na ubingwa wa Carabao Cup msimu huu. Kwa sasa wanafukuzia ufalme wa UEFA na wameratibiwa kuvaana na Real Madrid kwenye fainali ya Mei 28, 2022 jijini Paris, Ufaransa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Barbara Waweru ‘Mama Nyambu’ ni mwigizaji...

TAHARIRI: Kuwe na mfumo wa kuwekeza zaidi katika elimu ya...

T L