Michezo

Makocha wa Zoo Youth na APs Bomet walenga makubwa

April 10th, 2019 2 min read

Na JOHN KIMWERE

KOCHA wa Zoo Youth, Dominic Ochieng ameelezea matumaini ya timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano ya Kundi B Ligi ya Taifa Daraja la Pili na kuzoa tiketi ya kufuzu kushiriki Supa Ligi ya Taifa (NSL) msimu ujao. Kocha huyo alifunguka hayo baada ya kikosi hicho kuangusha GFE 105 kwa mabao 2-0.

”Wachezaji wangu wana furaha tele maana wanaendelea kujiongezea tumaini la kusonga mbele,” alisema na kuongeza kuwa dalili tayari zimeanza kuonekana.

Zoo Youth ilishuka dimbani kwa kusudio moja kutesa wenyeji wao na kuzoa alama tatu azma iliyotimiza kupitia mabao ya Peter Joma na Walter Otieno. Nayo Bungoma Superstars ya kocha, Ibrahim Shikanda ilikomoa Transfoc FC kwa bao 1-0 na kuendelea kukaa kifua mbele kwa kukusanya pointi 30, tatu mbele ya Zoo Kericho.

Katika mechi zingine, Vihiga Bullets iliendelea kufunga tatu bora kwa alama 25, tano mbele ya Egerton FC ilipobeba bao 1-0 mbele ya Raiply FC. Matokeo mengine, Kisumu Allstars ilidondosha pointi tatu ilipolala kwa mabao 2-0 mbele ya Silibwet FC nayo APs Bomet ilitoka sare tasa na Transmara Sugar.

Kama ilivyo kwenye mechi za kuwania ligi tofauti nchini, kipute hicho kushuhudia upinzani mkali. Bungoma Superstars ilishangaza wapinzani wao ilipobamiza AFC Leopards kwenye mechi ya 2019 SportPesa Shield Cup wiki mbili zilizopita.

Wachezaji wa Transfoc FC wakipasha misuli kabla ya kushuka dimbani kwenye mojawapo kati ya mechi za Kundi B Ligi ya Taifa Daraja ya Kwanza. Kwenye kampeni hizo Transfoc ilijikuta njia panda ilipolazwa bao 1-0 na Bungoma Superstars. Picha/ John Kmwere

Naye kocha wa Maafande wa APs Bomet, Sebastian Owino akizungumza na Dijitali alisema, “Ingawa tumekamata tano bora kwenye jedwali kwa kuzoa alama 16 bado hatujavunjika moyo tumepania kweli na kufuzu kupandishwa ngazi kushiriki kipute cha Supa Ligi ya Taifa (NSL).”

KOCHA wa maafande wa APs Bomet Sebastian Owino amesema wamepania kuonyesha ubabe wao kwa kupiga shughuli safi ili kufukuzia tiketi ya kupandishwa ngazi kushiriki Supa Ligi ya Taifa (NSL) msimu ujao.

Alisema haya baada ya wachana nyavu hao kutoka nguvu sawa bao 1-1 na Egerton University FC kwenye mechi ya Kundi B Ligi ya Taifa Daraja ya Pili iliyoandaliwa Silibwet Stadium. ‘

‘Mechi za msimu huu siyo rahisi tayari zimeashiria kuwepo ushindani mkali ambapo lazima tujitume ili tuwapiku mahasimu wetu,” alisema na kuongeza wanataka kumaliza kileleni ili kutuzwa tiketi ya kusonga mbele. Chini ya nahodha Ramadhan Ali, APs Bomet ilitangul