Habari Mseto

Malala na Savula wamkosoa Oparanya

August 10th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Gavana wa Kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya amekosolewa na marafiki wake wa zamani wake wanaomlaumu kwa kuwatupa wakazi wa Kakamega.

Seneta wa Kakamega Cleophas Malala na wabunge Ayub Savula wa eneobunge ya Lugari na Titus Khamala wa Lugari wamekuwa wakikosoa uongozi wa Gavana Oparanya jambo ambao umezua tofauti za kisiasa.

Maandamano yaliopangwa yawe Jumatatu na wafanya biashara yalisimamishwa dakika ya mwisho baada ya Bw Savula kusema kwamba alikuwa anapanga kushtaki serikali ya kaunti hiyo kwa kubomoa vibanda.

“Nimeagiza mwanasheria kuangalia maneno hayo ili waliopoteza mali yao wafidiwe,” alisema Bw Savula.

Bw Malala na Bw Savula wote ni wanachama wa chama cha ANCna wote walisema kwamba watakua wakiwania kiti cha ugavana ili kumrithi Gavana Oparanya na wamekuewa wakikosoa serikali ya Bw Oparanya.

Sewneta Malala alichochea wananchi wafanye maandamano baada ya serikali ya kaunti kubomoa vibanda vyao.