Na MASHIRIKA
SERIKALI ya Malawi imemwandikia barua bingwa wa zamani wa ndondi Mike Tyson, 54, ikimsihi akubali kuwa balozi wake wa zao la bangi.
Waziri wa Kilimo Lobin Lowe alisema kuhalalishwa kwa bangi nchini humo mnamo 2020 kumeibua fursa mpya ya biashara, na Malawi inalenga kujipa mapato.“Malawi huenda ikakosa kunufaika kikamilifu kutokana na biashara ya bangi iwapo itakosa kushirikiana na wadau wengine.
“Kwa hivyo, ningependa kukuteua Bw Mike Tyson uwe balozi wa sekta ya biashara ya bangi wa Malawi,” Lowe aliandika.Mwanandondi huyo wa zamani amekuwa akikuza na kuuza bangi tangu 2016.Kulingana na ripoti, Tyson, 54, amekuwa akijipatia Sh100 milioni kila mwezi kutokana na bangi.