MALEZI KIDIJITALI: Mipaka idumu hata mtoto akiwa kwa ‘ex’ wako

MALEZI KIDIJITALI: Mipaka idumu hata mtoto akiwa kwa ‘ex’ wako

MZAZI anapaswa kuweka mipaka kati ya mtoto wake na mzazi mwenza wasiyeishi pamoja iwapo anahisi kuna sababu ya kufanya hivyo hata baada ya kufanikisha mawasiliano na ‘ex’ wake.

Hata hivyo, wataalamu wanasema kwa kuweka mipaka hiyo, mzazi anapaswa kuacha nafasi ya kulegeza msimamo kwa kutambua mchango wa mzazi mwenza kwa maisha ya mtoto, iwapo tu anajua hauathiri usalama na maadili ya mwanawe.

“Mipaka mizuri ni ile ambayo kila mmoja anaweza kukubaliana nayo; hata hivyo, kama mzazi unayeishi na mtoto una haki ya kushikilia mipaka hata kama watoto wako na ex wako hawakubaliani nayo mradi tu unaelewa na una hakika haitaumiza mtoto,” wasema wataalamu wa tovuti ya www.defendyounminds.com.

Kulingana na wataalamu hao wa malezi dijitali, mipaka inatumiwa kwa usalama na iwapo watu wengine hawatambui haja ya kuhakikisha usalama huo, tumia mipaka hiyo kuwadhihirishia wazi mtoto wako anapaswa kuwa salama.

“Ukijua mipaka unayopaswa kuweka, chunguza anachotaka ex wako na hata mtoto. Kabla ya kufanya hivi, ni lazima uwe umejenga mawasiliano na wahusika. Kila kitu wanachopendekeza na unachojua ni kizuri, kikubali na ukisherehekee,” wanasema wataalamu hao.

Baadhi ya mpaka ambayo watalaamu wa malezi dijitali wanashauri wazazi kumakinikia ni kutenga watoto na vifaa bebe katika maeneo yao ya kibinafsi kama vyumba vya kulala, bafu au wakiwa peke yao nyumbani na mzazi na mzazi mwenza kutotumia vifaa bebe katika vikao vyao vya pamoja na mtoto wao.

“Mipaka mizuri inaweza kuleta mambo mazuri, mbali na kuwa marufuku tu,” wanaeleza wataalamu hao na kusisitiza kuwa ni muhimu wazazi waweze kuizingatia.

Kulingana na tovuti hiyo, wakati wa kutumia vifaa bebe unapaswa kuwa baada ya majukumu ambayo wazazi wanapatia watoto kwa kuzingatia haki zao.

“Watoto wanafaa kutangamana na vifaa vya dijitali baada ya kufanya kazi za shuleni na za nyumbani. Pia, wanafaa kupakua apu zozote katika vifaa bebe kwa idhini ya mzazi pekee,” wanasema na kusisitiza mzazi hafai kulegeza msimamo kuhusu mipaka kwa shinikizo za mzazi mwenza.

  • Tags

You can share this post!

PENZI LA KIJANJA: Ikiwa mnapendana, msisahau busu kwani...

Azimio yaonya polisi kuhusu maandamano

T L