Habari Mseto

Mali ya Sh5 milioni yateketea Isiolo

August 10th, 2020 1 min read

WAWERU WAIRIMU na FAUSTINE NGILA

Mali ya thamani ya mamilioni ilih aribiwa na moto Ijumaa kwenye karakana moja kwenye chuo cha ufundi cha St Joseph mji wa Isiolo.

Bw Steve Mathenge, anayeishi kwenye kanisa la Katoliki la Isiolo mabapo chuo hicho kimejengwa alisema kwamba aliona moshi ukitoka kwenye karakana hiyo na akatoa habari hizo kwa maafisa wa usalama.

Padri Jerewmy Murithi alisema kwamba mali ya zaidi ya Sh5 milioni iliharibiwa huku moto huo ukihusishwa na umeme.

Kulingana na Padri Murithi, juhudi za wafanyakazi wa kanisa na timu ya kupigana na mikasa ya moto ya kauntin a wakazi walifanikiwa kuzima moto huo ambao ulikuwa umesambaa karibu na chumba kilichokuwa na mitungi ya gesi.

“Moto huo ulitokana na umeme baada ya maji ya mvua kuingia kwenye tundu la paa,” alisema Padri Murithi.

BI Pauline Kinyua, afisa wa maswala ya usalama wa watoto kwenye kanisa hilo alishukuru timu ya kupambana na mikasa ya moto ya kaunti kwa kuitikia wito wao kwa haraka.