Habari Mseto

Malimwengu jamaa akiacha mkewe kitandani na kwenda kufanya ngono na mbwa

February 26th, 2024 1 min read

NA WYCLIFFE NYABERI 

MWANAUME mmoja katika Kaunti ya Kisii, amewashtua wakazi baada ya kumwacha mkewe kitandani na kwenda kufanya kitendo cha ngono na mbwa wao.

Tukio hilo la kustaajabisha lilifanyika usiku wa Jumapili, Februari 25, 2024 sehemu za Mosocho eneobunge la Kitutu Chache Kusini.

Kulingana na ripoti aliyoandikisha Bi Alice Kwamboka, 40, katika kituo cha polisi cha Mosocho, mumewe Fredrick Macarios, 60, alimngoja apate usingizi kabla ya kutoka nje na kuanza kufanya kitendo hicho.

Lakini mwanamke huyo aliamshwa na kelele ya mbwa wao kwa jina “Poster“.

Baada ya kumkosa mume wake kitandani, Bi Kwamboka alitoka nje kujua kilichokuwa kikimliza mbwa huyo na hapo ndipo alimpata mume wake “anashiriki mapenzi” na mnyama huyo wa kike.

“Bi Kwamboka aliwaamsha wanafamilia wengine walioshuhudia kisa hicho,” ilisema sehemu ya ripoti ya polisi kuhusu malimwengu hayo.

Maafisa wa polisi na wale wa mifugo walizuru boma hilo na kumkamata mwanaume huyo ili kumchukulia hatua zinazofaa.

Tukio hilo linajiri siku chache tu baada ya mwanaume mwingine kujifanya mwanamke ili kumwibia mteja wake simu katika klabu kimoja eneo la Nyamataro.