Kimataifa

Malkia Elizabeth atuza kahaba kwa 'mchango wake katika ngono'

June 5th, 2018 1 min read

Na AFP

KAHABA mmoja wa zamani nchini Uingereza Jumatatu alituzwa na Malkia Elizabeth nchini New Zealand “kwa mchango wake katika biashara ya ngono.”

Catherine Haealy alichangia pakubwa katika harakati za kuondoa dhana ya ukahaba kuorodheshwa kuwa uhalifu mnamo 2003.

Aidha, alichangia hayo kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo katika nchi kadhaa duniani.

Hata hivyo, Catherine ambaye ana umri wa miaka 62, alisema kwamba hakutarajia kulipata. “Sikutarajia tunzo kubwa kama hili. Ningali katika hali ya mshangao,” akasema, kwenye mahojiano na kituo cha Radio New Zealand. Kinyume na hayo, alisema kwamba alitarajia kukamatwa.

“Ni heshima kubwa sana kwangu,” akasema. Haealy amekuwa akiongoza harakati za kutambuliwa kwa ukahaba kama biashara huru tangu 1989. Harakati hizo pia zinajumuisha utambuzi wa haki za makahaba na malipo mazuri kwa “huduma” wanazotoa kwa wateja wao.

Amesema kwamba anaamini kwamba harakati zake zimezaa matunda, kwani kwa sasa, nchi nyingi zinawatambua makahaba na kuzingatia haki zao kama wafanyakazi wengine.

Kutokana na utambuzi huo, ameapa kuhakikisha kwamba ameongeza harakati zake.