Malumbano makali kati ya mawakili na DPP kuhusu kesi ya Sh8Milioni

Malumbano makali kati ya mawakili na DPP kuhusu kesi ya Sh8Milioni

Na RICHARD MUNGUTI

MZOZO mkali ulizuka kati ya mawakili wanaowakilisha wakurugenzi watano wa kampuni ya kuuza mafuta na mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Mawakili Emily Nyongesa na Bw  Danstan Omari wanaowakilisha Doreen Emily Akinyi Otieno , Thayu Kamau Kabugi na Michael Kanuthu Pompirio waliteta mbele ya hakimu mwandamizi kwamba wateja wao waliagizwa wafike kortini ilhali hakuna faili ya kuwashtaki.

Watatu hawa pamoja na  Christopher Bwakali Arthur na Boniface Mayabi Nasongo wanadaiwa walifuja kampuni ya BeEnergy bidhaa za mafuta ya petrol ya Sh8milioni.Washtakiwa hao waliagiza bidhaa za mafuta ya petroli ya kuuza nje lakini wakayauza humu nchini.

Kampuni ya BeEnergy ilitozwa faini ya Sh8milioni na mamlaka ya ushuru nchini kwa kuruhusu mafuta ya kuuzwa nje ya Kenya kuuuziwa wateja humu nchini.Kiongozi wa mashtaka alisema kesi hiyo yapasa kusikizwa na mahakama ya Kisumu.

Lakini wakili Omari alisema mshtakiwa anaweza kushtakiwa mahala popote.“Kuna ushahidi kwamba mshukiwa anaweza kushtakiwa popote Kisumu , Mombasa Nairobi na hata Kitale.

Washtakiwa hawa wamefika kortini wasomewe mashtaka wajue hatma yao,” alisema Bw Omari.Lakini kiongozi wa mashtaka Bw James Machira aliomba muda apate maagizo zaidi kwa vile kesi hiyo ingelisikizwa na  mahakama ya Kisumu.

Pia alisema idara ya kupambana na ufisadi yapasa kushughulikia kesi hiyo.“Inaonekana afisi ya DPP imechanganyikiwa. Mbona iwasilishe kesi ya kitengo cha EACC katika mahakama ya kuamua kesi za kawaida,” alisema hakimu mwandamizii Bw Bernard Ochoi.

Bw Omari alisema ni jambo la kufedhehesha sana ikiwa afisi ya DPP iliwasilisha kesi dhidi ya washtakiwa kama hakuna faili.Hata hivyo kiongoz wa mashtaka Bw James Machira alijibu akisema makosa yalifanyika wakati kesi hiyo ilipowasilishwa mbele ya hakimu mwandamizi Bw Bernard Ochoi badala ya kupelekwa kitengo cha kuamua kesi za ufisadi.

“Naungama kwamba makosa yalifanyika washtakiwa kuagizwa wafike kortini ilhali hakuna faili yao iliyowasilishwa kortini,” Bw Machira.Mahakama iliamuru kesi hiyo itajwe Septemba 22, 2021.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Kukabili athari za tabianchi: Denmark mfano...

Mkakati wangu ni wa kuleta maendeleo na amani – Ruto