Dondoo

Mama aliyeenda kwa mganga amsaidie kuponyoka na mume wa wenyewe atimuliwa kiaibu

April 27th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

MGANGA wa hapa alimtimua demu aliyefika kwake akitaka ampe hirizi atumie kujishindia mume wa mwanadada mwingine.

Demu alikuwa akimezea mate jamaa ambaye ana mke na mtoto mmoja na mistari yake ilipogonga mwamba akaamua kutafuta ndumba kutoka kwa mganga.

Alipomweleza mganga huduma alizotaka, babu alimkemea vikali.

“Siwezi kukusaidia kunyang’anya mtu mwingine mume wake. Koma kabisa kutamani waume wa wake wengine na utafute wako,” mganga alimwambia demu.

Duru zinasema mwanadada alijaribu kukwamilia kwa mganga lakini akafurushwa.

“Toka. Ondoka na usiwahi kurudi hapa ukitaka huduma kama hiyo,” mganga alifoka.