Habari Mseto

Mama ashuku mwanawe hakujitia kitanzi

August 10th, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE na FAUSTINE NGILA

Kijana wa mika 11 alipatikana amefariki Jumapili kwenye kijiji cha Kaitheri kaunti ya Kirinyaga katika kile kinachoaminika kuwa kisa cha kujitia kitanzi.

Mwili wake ulipatikana umeninginia kwenye paa la nyumba ya wazazi wake asubuhi.

Mama yake alisema kwamba alikuwa kwenye hoteli anapofanya kazi alipopata habari hizo za kifo cha mwanawe.

“Nilipopata habari hizo nilikimbia na nikapata kijana wangu akiwa amefariki na akiwa na waya waumeme shingoni mwake,” alisema.

Alisema kwamba alishuku kuna mbinu chafu na akaita maafisa wa DCI kufanya uchunguzi. “Nilishtuka nilipoona mwili wa mtoto wangu. Inakisiwa akijitia kitazi lakini nashuku,” alisema.

Chifu msaidizi Katheri Kepha alisema kwamba juhudi zao za kuokoa maisha ya kijana huyo ziliambulia patupu.

“Niliambiwa kwamba baba ya kijana huyo alijaribu kuokoa maisha ya kijana huyo ikashindikana,” Bw Maricho alisema.

Afisa huyo alisema kwamba alikuwa nyumbani alipopokea habari hizo na alienda kwenye eneo hilo na akakuta kijana huyo akiwa tayari amefariki.

Mwili huo ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Kerugoya.