Habari Mseto

Mama atupwa ndani kwa kuchoma mtoto

August 8th, 2020 1 min read

BENSON AMADALA na FAUSTINE NGILA

Mwanamke aliyemchoma mwanawe wa miaka minane kwa sababu ya mlo wa chapati amefungiwa kwenye kituo cha polisi cha Matete, Kaunti ya Kakamega.

Mwanamke huyo alimfunga mwanawe kwa kutumia nywele pana baada ya kumchoma kwa mafuta taa.

Mshukiwa huyo wa miaka 38 alikamatwa baada ya majirani kuripoti kwamba alikuwa ameumiza mwanawe akimlaumu kwa kukula chapatti mbili alizokuwa ametengeneza.

Kijana huyo alikuwa ameenda kucheza na wezake aliporudi jioni nyumbani Jumatano ndio mamayake akimpa kichapo cha ubwa.

“Mamayangu alinivuruta na akaniagiza nitoe nguo na ku nichapa kabla ya katumia nywele kunifunga mikono na kunichoma kwa mafuta taa,”alisema kijana huyo.

Kijana huyo alifanikiwa kutoroka na kuripoti kwa jirani moja ambaye alienda kuchunguza kilichotokea.

Majirani walioshangazwa na tukio hilo walisema kwamba mwanamke huyo amekuwa akimtesa kijana huyo baada ya kutofautiana na bwanake.

Alikuwa amekamatwa baada ya kuchoma kijana huyo kwa chuma moto.

Bw Mukongolo na bibyake walisema kwamba kijana huyo alikua anateswa sana na mamayake na alikuwa nahitaji usaindizi.