Kimataifa

Mama aumizwa na kemikali ya kusisimua uume aliyopaka kwa jicho

January 9th, 2019 1 min read

MASHIRIKA na PETER MBURU

MWANAMKE aliyekuwa akiugua jicho alipata majeraha mabaya katika sehemu hiyo ya mwili wakati alipoenda hospitalini kutafuta matibabu, lakini badala ya kupewa dawa inayofaa akapewa mafuta ya kupaka kusisimua uume.

Mgonjwa huyo kutoka Glasgow alikuwa akitibiwa katika hospitali ya A&E, wakati kimakosa alipewa mafuta hayo ya Vitaros badala ya yale ya VitA-POS, shirika moja la habari likasema.

Baada ya kutumia mafuta hayo katika jicho lake, aliathirika vibaya na kemikali iliyoko ndani yake hadi akaanza kuwa na matatizo ya kuona na jicho kuanza kufura.

Hali hiyo ilifanya wataalam wa udaktari Glasgow kuwataka madaktari kuwa makini pale wanapotoa matibabu.

“Inashangaza katika kisa hiki kuwa hakuna mtu yeyote, ikiwemo mgonjwa ambaye alitambua kuwa mafuta hayo ni ya kutibu shida za nguvu za kiume, na yalikuwa ya mwanamke,” akasema Dkt Magdalena Edington.

Baadaye, mwanamke huyo alitibiwa kwa majeraha aliyopata kwa haraka, japo wataalam wakisisitiza kuwa madaktari wawe makini wanapotoa dawa kwa wagonjwa.