Habari Mseto

Mama awasamehe vijana walioharibu mimea yake na kuiba hela

June 11th, 2020 1 min read

Na  CHARLES WANYORO

Mkulima mmoja amebatilisha azma ya kuwashtaki vijana tisa wanaoaminika kuwa miongoni mwa genge lililovamia na kubomoa nyumba yake na kuharibu mimea yake shambani katika Kijiji cha Mwereru kaunti ya Meru.

Bi Mary Mwiti aliwalaumu vijana hao kwa kufanya kosa hilo huku wakimtishia kwa panga baada ya kuwaonya kwa sababu ya kumchapa mwanawe Dennis Koome Mwiti.

Vijana zaidi ya 50 walimlaumu Bi Mwiti kwa kutenda kinyume na utamanduni wa jamii ya Wameru unaonyima wanawake kuwatetesha vijana waliotairiwa hivi karibuni.

Mwezi jana vijana hao waliokana kukatakata ndizi, viazi, mchicha vyenye thamani ya Sh18,700, kubomoa nyumba na kuiba Sh8,000 waliachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 kila mmoja mbele ya hakimu mkuu.

Wakili wa serikali aliiambia mahakama kwamba vijana hao walichukua Sh8,000 kutoka kwa Bi Mwiti huku wakitishia kubomoa nyumba ingine.

Alhamisi Bi mwiti aliiambia korti kwamba alikuwa amewasamehe vijana hao ambao wana miaka 25 na chini.

Tafsiri: Faustine Ngila