Mama mboga ‘aoza’ binti kwa mteja wa kila siku

Mama mboga ‘aoza’ binti kwa mteja wa kila siku

Na TOBBIE WEKESA

BUNYALA, BUSIA

MAMA mboga wa eneo la hapa aliwaacha wengi vinywa wazi alipompa polo binti yake kama zawadi.

Inasemekana polo alikuwa mteja mkubwa wa mama mboga na inadaiwa mama huyo alianza kumchunguza kubaini ikiwa alikuwa na mke.

Alifaulu kubaini kwamba polo hakuwa ameoa.

Inadaiwa jioni moja mama mboga aliamua kufungua roho.

“Kila siku wewe huja kununua mboga kwangu. Kazi hii ni ya wanawake. Kwani huna mke?” polo aliulizwa huku mama akimwambia kuwa hafai kuchoka kwenda kununua mboga na kujipikia.

“Mama usijali. Muda wangu wa kuasi ukapera utafika tu. Mungu atanipa mke mwema,” polo alijitetea.

Habari zilizotufikia zinasema mama mboga alimpigia simu binti yake akafika mara moja.

“Huyu ni binti yangu. Nakupa zawadi ya bure. Atakuwa mkeo. Atakushughulikia kwa hali zote. Ni mke unayesubiri kutoka kwa Mungu,” mama mboga alimueleza polo.

You can share this post!

Ni Ruto au Raila? PAA yajipata ikijikuna kichwa

CECIL ODONGO: Kina mama wajitokeze na kusaka kura bila...

T L