Kimataifa

Mama taabani kwa kukubali Sh40,000 bintiye anajisiwe na babu

May 15th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU
 
MWANAMKE kutoka Texas amekamatwa na polisi, baada ya kushirikiana na mwanamume wa miaka 62 ili amnajisi mwanawe wa miaka mitano, baada ya kulipwa Sh40, 000.
 
Shirley Harmon, 36, wa kutoka eneo la Odessa alikamatwa Jumapili na polisi, kisha akafunguliwa mashtaka ya kushirikiana kudhulumu mtoto.
 
Mwanamke huyo aliripotiwa kuwa alikiri mbele ya polisi waliokuwa wakichunguza kesi hiyo kuwa alimruhusu Gary Landreth, wa miaka 62 kumnajisi mwanawe kati ya 2017 na 2019.
 
Polisi walisema wawili hao walianza kumdhulumu mtoto huyo alipokuwa na miaka miwili tu.
 
Landreth alikamatwa Januari 14, lakini akaachiliwa kwa bondi ya Sh5 milioni.
 
Polisi walisema mtoto huyo alipopimwa ikiwa alikuwa amenajisiwa, kifaa cha kumpima kilionyesha kuwa ni kweli alitendewa unyama huo.
 
Harmon alieleza wachunguzi kuwa bintiye alimwambia mshukiwa alikuwa na hulka ya kumgusa isivyofaa na kumuumiza kila mara walipoachwa naye, karatasi za korti zimesema.
 
Lakini wachunguzi wanasema Harmon hakusikia kilio cha mwanawe, akimuacha Landreth kuendelea kumdhulumu.
 
Polisi walisema Harmon alikiri kuwa alipokea Sh40,000 kutoka kwa Landreth ili kumruhusu aendelee na tabia hiyo.
 
Mwanamke huyo aliachiliwa kwa bondo ya Sh5 milioni lakini bado yuko seli baada ya kukosa.