Mama taabani kwa kuchoma matiti ya mwenzake

Mama taabani kwa kuchoma matiti ya mwenzake

Na PETER MBURU

MWANAMKE wa miaka 52 alishtakiwa Jumanne kwa kuchoma matiti ya mwenzake, kwa kuwa mwanaye mdhulumiwa alimwita ‘mapengo’.

Bi Betty Nabwire Nakhulo anadaiwa kumchoma Bi Sarah Atieno kifuani mnamo Agosti 18, na kumjeruhi vibaya.

Kulingana na polisi, mshukiwa alimvamia Bi Atieno ambaye ni jirani yake nyumbani kwake na kumtendea unyama huo, akidai mwanawe alimwita mapengo.

Polisi walisema mshukiwa alilalamika kwa mumewe Bi Atieno, akielezea haswa ghadhabu yake kwa kuitwa mapengo na mtoto.

Korti ilizidi kufahamishwa kuwa aliporudi nyumbani, Bi Atieno ambaye hakuwepo alipoingia Bi Nabwire alimpata mshukiwa akimzomea mumewe na kuzua fujo.

Korti ilisikia namna Bi Atieno alianza kumlaumu jirani yake kuwa anayeiba waume za watu, akisema hakuwa na ruhusa yoyote wala msingi kuwazomea kuhusu uzazi.

Lakini mshukiwa anasemekana kuchukulia maneno hayo kwa uzito, na baada ya kubishana kwa muda mfupi akapanda mori na kuchukua sufuria iliyokuwa na maji moto jikoni na kumwosha Bi Atieno.

Katika kisa hicho, korti ilielezwa Bi Atieno alijeruhiwa titi la kushoto kisha mshukiwa akatoroka.

Mdhulumiwa alikimbizwa hospitalini baadaye.

Bi Nabwire alikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh100,000 pesa taslimu, huku kesi hiyo ikiratibiwa kusikizwa Novemba 28.

You can share this post!

Najivunia makalio yangu, seneta akana kudai huduma ghali za...

Daktari motoni mahakama kusimuliwa alivyotekeleza mauaji

adminleo