Habari Mseto

Mama taabani kwa kuwachoma wanawe kwa upanga moto

January 7th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE aliyewafanyia unyama wanawe wawili kuwa kuwachoma kwa upanga moto ameshtakiwa.

Huku akiwa na hasira za mkizi na kupangawa pepo mbaya kana kwamba sio aliyewazaa mama huyo alichukua upanga na kuutia kwenye moto na ulipata joto kabisa alianza kuwatia adhabu kwa kuwachoma huku akiwakemea.

Mahakama ilielezwa kuwa watoto hao walifakamia chakula hicho kwa sababu ya njaa na kujituliza nacho bila idhini.

Ijumaa Joyce Nyambura alifikishwa mbele ya hakimu mkazi mahakama ya Narok Hosea Ng’ang’a na kufunguliwa mashtaka ya kuwajeruhi wanawe wawili wenye umri wa miaka tisa na 13 mtawalia mnamo Desemba 10, 2018.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la Nairegie Enkare, katika kaunti ndogo ya Narok Mashariki.

Afisa wa urekebishaji tabia katika eneo la Narok Kaskazini Amanda Chesiyna aliiambia mahakama kwamba wavulana hao wawili walitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Narok na sasa wameripoti shuleni.

“Katika kipindi ambapo mamake alikuwa kizuizini, watoto hao pamoja na baba yao walikuwa wakimtembelea kumjulia hali. Waliiomba mahakama kumwachilia huru ili aungane nao nyumbani,” Bi Chesiyna akaambia mahakama.

Katika ripoti yake, afisa huyo anasema kuwa baba ya watoto hao Timothy Ndung’u amemfichulia kuwa mkewe hakukusudia kutenda kosa hili kwani ni mama anayewapenda wanawe na nguzo katika familia hiyo  ya watoto watano.

Kesi hiyo itatajwa mnamo Januari 16, 2019 na kutajwa mnamo Machi 14, 2019.