Mama wa kambo alinifinya nyeti, mwanaume alilia korti

Mama wa kambo alinifinya nyeti, mwanaume alilia korti

NA BRIAN OCHARO

MWANAMUME mmoja aliwaacha watu vinywa wazi alipolia mahakamani kuwa alifinywa sehemu nyeti na mamake wa kambo baada ya kutofautiana.

Bw Eddie Okumu Ratiel aliiambia Hakimu Mkuu wa Mombasa Martha Mutuku kuwa alisikia uchungu na kumsukuma mwanamke huyo.

“Mimi sikumpiga lakini ni ukweli kuwa nilimsukuma aliponifinya. Nilihisi uchungu kwa hivyo singeweza kuvumilia ndipo nikamsukuma aniondokee,” alisema jamaa huyo.

Pia, aliiambia mahakama kuwa kando na kufinywa nyeti, mwanamke huyo alimuuma na kumsababishia jeraha la mkono.

“Naomba mahakama iamuru nipelekwe hospitali nikatibiwe. Nahofia kuambukizwa magonjwa yanayotokana na bakteria,” alisema.

Bw Okumu anakabiliwa na mashtaka mawili ya kupiga mtu kinyume na sheria.

Hakimu Mutuku aliamuru jamaa huyo apelekwe hospitali kwa matibabu.

Kesi hiyo itatajwa tena Disemba 7.

  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Qatar yadenguliwa baada ya...

TUSIJE TUKASAHAU: Mpango wa madereva na makondakta kupokea...

T L