Habari Mseto

Mama yake Naibu Waziri apatikana na corona

November 10th, 2020 1 min read

LILLIAN MUTAVI NA FAUSTINE NGILA

Spika wa Kaunti ya Machakos Florence Muoti Mwangangi alipatikana na virusi vya corona.

Mama yake Katibu Naibu Waziri katika Wizara ya Afya Mercy Mwangangi alisema kwamba alikuwa karantini baada ya kupimwa.

” Hii ni siku ya tisa tangu niambukizwe virusi vya corona na siwezi juaa niliipata kutoka wapi ata baada ya kujikinga,”alisema Jumapili.

Spika huyo alisema kwamba hali yake inaendelea kuwa sawa kwani amepata nafuu ata kama dalili za corona zinaongezeka wakakti mwingine.

Alisema kwa,mba alianza kujishuku baada ya mwezake kupata dalili za homa.

“Niliona mwezangu akiwa na dalili za homa hapo ndipo tuliamua kwenda kupimwa,”alisema Spika Mwangangi.Walipatikana na virusi vya corona.

Aliomba wananchi wajikinge na corona kwani corona ni ya ukweli akisema kwamba lipata virusi hivyo ata baada ya kufuata maangizo yaliyotolewa na wizara ya afya.Aliwaomba watu wengine ambao waliopata virusi vya corona wajitokeze kuogelela kuhusu corona.na wasiogope.

Akizungumzia kuhusiana kuhusiana na dalili za corona alisema kwamba kila siku ni tofauti na dalili.Aliomba wale ambao ni wagonjwa wajipe moyo na wawe na wawe na Imani.