Mamaye Hamisa alia bintiye kuitwa ‘wa kando’ na Diamond

Mamaye Hamisa alia bintiye kuitwa ‘wa kando’ na Diamond

Na PETER MBURU

MSANII Diamond Platnumz kutoka Bongo aliibua cheche za maneno pale alipomrejelea kichuna Hamisa Mobetto kuwa ‘wa kando’, na mwanaye Dylan kuwa ‘mwanaharamu’ kwenye video iliyosambaa mitandaoni.

Katika video hiyo inayodaiwa kuwa ya mahojiano kati ya Diamond akiwa Nigeria, msanii huyo anasikika akijilaumu kuwa 2017 ulikuwa mwaka mbaya kwake.

Alisema ni mwaka huo ambapo alichezea penzi lake na mpenzi wake wa muda mrefu Zari Hassan, na Hamisa Mobetto.

Mwishoni mwa kanda hiyo, Diamond anawashauri watu walio na mipango ya kando kuwa makini na wawe wakitumia kondomu ili kuzuia kuwapa mimba mipango ya kando kama alivyofanya yeye.

Lakini semi hizi za msanii huyo hazikupokelewa vyema na mamake Hamisa Mobetto, Bi Shufaa Lutiginga, ambaye sasa amesema zilimchoma rohoni.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Bi Shufaa alisema hangependa hata kuyasikia mambo hayo tena kutokana na uchungu yaliyompa.

“Jamani inauma na kwa kweli nisingependa hayo mambo jamani kuyaongelea mimi… jamani naombeni sana mtafuteni huyo mwenyewe aliyesema au Mobeto tafadhali, niacheni mimi nipumzike,” akasema Bi Shufaa.

You can share this post!

Mtoto ajiua kwa kusimangwa kuwa shoga

Najivunia makalio yangu, seneta akana kudai huduma ghali za...

adminleo