Michezo

Mamaye Neymar,52, amuonjesha asali kijana wa miaka 22

April 19th, 2020 2 min read

MASHIRIKA Na CHRIS ADUNGO

NADINE GONCALVES/TIAGO RAMOS

NADINE Goncalves, 52, ambaye ni mamaye sogora Neymar Jr wa Paris Saint-Germain (PSG), amekuwa gumzo ndani nje ya taifa la Brazil baada ya kubainika kwamba anatoka kimapenzi na Tiago Ramos – kijana mdogo wa umri wa miaka 22 ambaye ni shabiki sugu wa michezo ya kompyuta.

Neymar, 28, anamshinda mpenzi mpya wa mama yake kwa umri wa miaka sita zaidi.

Mwishoni mwa wiki jana, Nadine alipasua mbarika kuhusu uhusiano wa siri wa miaka miwili ambao amekuwa nao na Ramos. Akitumia mtandao wake wa Instagram, alipakia picha walizowahi kupigwa katika sehemu mbalimbali za burudani wakiponda raha.

Katika mojawapo ya picha hizo, Nadine alikuwa amekishika kidevu cha Ramos aliyekuwa akipapasa maziwa ya nyanya huyo huku akimpiga mabusu motomoto.

Chini ya picha hizo, Nadine aliambatisha maneno, “Haya yaliyotokea hayawezi kufafanuliwa zaidi yakaeleweka kwa wasiojua maana ya nguvu za mapenzi. Ishini kutuvumilia,” akasema Nadine.

Kwa mujibu wa gazeti la UEL Esporte nchini Brazil, Ramos ni mpenzi kindakindaki wa masuala ya kompyuta na sehemu ya kikosi cha 4K Easy kinachojulikana kwa umaarufu wa kuunda michezo ya kompyuta.

Nadine alitengana na Wagner Ribeiro ambaye ni baba na wakala wa Neymar mnamo 2016 baada ya kuishi pamoja katika ndoa kwa kipindi cha miaka 25.

Licha ya ukubwa wa pengo la miaka katika umri wa Nadine na Ramos, Neymar ameonekana kuunga mkono uhusiano mpya wa mamaye.

“Kula raha mama. Nakupenda sana,” akaandika Neymar katika kauli iliyoonekana kuungwa mkono na Ribeiro.

Hadi walipoanza kulitomasa tunda la Nadine mnamo 2018, Ramos ambaye ni mzawa wa mji wa Pernambuco nchini Brazil, alikuwa shabiki sugu wa Neymar huku akihudhuria takriban michuano yote iliyomhusisha nyota huyo wa zamani wa Barcelona.

Kwa upande wake, Neymar pia amekiri kujinasia penzi la mwanamitindo mzawa wa Cuba, Natalia Barulich, 28.

Neymar na Natalia wanaanza kutoka kimapenzi mwaka mmoja baada ya kipusa huyo raia wa Croatia, kutemana na mumewe Maluma. Maluma ni mwanamuziki maarufu mzawa wa Colombia, aliyewahi kunogesha hafla ya Neymar wakati akiadhimisha miaka 27 ya kuzaliwa.

Wiki iliyopita staa huyo alionekana akiponda raha na Natalia, ambaye duru zinasema pia anawaniwa na mwanasoka wa zamani wa Chelsea, John Terry, 39.

Tangu atemane na Maluma, Natalia amekuwa mwepesi wa kupakia picha za Neymar mtandaoni, akiambatisha jumbe zinazoashiria kuwepo kwa mapenzi kati yao.

“Kila mtu anafahamu ustadi wa kipaji chako uwanjani, ila wangejua ulivyo mtamu na ndani pia. Unazo heshima zangu zote mpenzi!” akaandika Natalia huku akitia alama za kuashiria mabusu mmwishoni mwa ujumbe huo.

Katika picha nyingine, Natalia alikuwa amevalia rinda jeupe ambalo alifichua kwamba lilinunuliwa na straika huyo mahiri mwishoni mwa mwaka jana walipokutana katika hafla moja jijini Rio, Brazil.

“Rinda hili ni zawadi tosha kutoka kwa Neymar, dume ambalo nalistahi sana kwa pendo la kweli,” akasema demu huyo.

Aidha, kidosho huyo amemtaka Neymar kukomesha kabisa mawasiliano ya mara kwa mara na wanamitindo Izabel Goulart na Alsessandra Ambrosio, waliowahi kumgawia tunda mwanzoni mwa 2019 jijini Dusseldorf, Ujerumani.

Neymar anaanza kumtambalia Natalia kimapenzi miezi michache baada ya kutengana na mwigizaji maarufu mzawa wa Mexico, Danna Paolo, 24.

Danna alikuwa kiini cha kuvurugika kwa uhusiano wa miaka sita kati ya Neymar na kichuna Bruna Marquezine, 24.

Awali, Neymar alikuwa akila bata na mwanamitindo Mari Tavares kabla ya kukiri kuvutiwa na maungo ya Ellen Santana, aliyetawazwa mshindi wa Miss BumBum nchini Brazil mnamo 2018.

Ni miezi sita tu imepita tangu nyota huyo atemane pia na mwanamitindo Noa Saez, aliyekuwa mwenyeji wake wa mara kwa mara katika mkahawa wa Mr Porter jijini Catalonia, Uhispania.

Noa aliingia katika orodha ndefu ya vichuna wa Neymar baada ya sogora huyo kutomasa pia matunda ya warembo Liza Brito kutoka Uswizi na Larissa ‘Anitta’ Macedo wa Brazil.