Man-City kukutana na PSG huku Liverpool wakitiwa katika zizi gumu la UEFA msimu huu

Man-City kukutana na PSG huku Liverpool wakitiwa katika zizi gumu la UEFA msimu huu

Na MASHIRIKA

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Manchester City, wametiwa katika Kundi A kwa pamoja na Paris Saint-Germain (PSG), RB Leipzig na Club Bruges kwenye kipute cha kuwania taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu huu wa 2021-22.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola (kushoto) akiwa ameshika Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya mechi ya Manchester City dhidi ya Everton uwanjani Etihad, Manchester, Mei 23, 2021. Picha/ AFP

Chelsea waliotwaa taji la UEFA mnamo 2020-21, wamepangwa katika Kundi H kwa pamoja na Juventus ya Italia, Zenit St Petersburg ya Urusi na Malmo ya Uswidi.

Straika wa Chelsea, Romelu Lukaku wakati wa mechi dhidi ya wenyeji Arsenal. Picha/ AFP

Manchester United watavaana na Villarreal ya Uhispania, Atalanta ya Italia na Young Boys kutoka Uswisi katika Kundi F. Villarreal wanaotiwa makali na kocha Unai Emery ndio waliwapiga Man-United kwenye fainali ya Europa League mnamo 2020-21.

Liverpool ambao ni wawakilishi wengine wa Uingereza kwenye kivumbi cha UEFA msimu huu, watakuwa na kibarua kizito kwenye Kundi B linalojumuisha pia Atletico Madrid ya Uhispania, FC Porto ya Ureno na AC Milan ya Italia.

Fainali ya UEFA msimu huu wa 2021-22 itaandaliwa jijini St Petersburg, Urusi mnamo Jumamosi ya Mei 28, 2022.

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City waliozidiwa maarifa na Chelsea kwenye fainali yao ya kwanza ya UEFA mnamo 2020-21, watalazimika kukabiliana na kibarua kigumu cha Kundi A kutoka kwa PSG wanaojivunia maarifa ya fowadi matata raia wa Argentina, Lionel Messi.

MAKUNDI YA UEFA 2021-22:

KUNDI A: Manchester City, Paris St-Germain, RB Leipzig, Club Bruges.

KUNDI B: Atletico Madrid, Liverpool, Porto, AC Milan

KUNDI C: Sporting Lisbon, Borussia Dortmund, Ajax, Besiktas.

KUNDI D: Inter Milan, Real Madrid, Shakhtar Donetsk, Sheriff Tiraspol.

KUNDI E: Bayern Munich, Barcelona, Benfica, Dynamo Kyiv.

KUNDI F: Villarreal, Manchester United, Atalanta, Young Boys.

KUNDI G: Lille, Sevilla, FC Salzburg, Wolfsburg

KUNDI H: Chelsea, Juventus, Zenit St Petersburg, Malmo.

You can share this post!

Real Madrid watoa ofa ya Sh21.3 bilioni kushawishi Kylian...

KCB Machakos Rally yavutia madereva 30