Man-City wang’oa Kalvin Phillips kambini mwa Leeds United ili kujaza nafasi ya Fernandinho

Man-City wang’oa Kalvin Phillips kambini mwa Leeds United ili kujaza nafasi ya Fernandinho

NA MASHIRIKA

MANCHESTER City wameafikiana na Leeds United kumsajili kiungo wa Uingereza, Kalvin Phillips kwa Sh6.6 bilioni ili kujaza pengo la kigogo Fernandinho Luiz Roza atakayeondoka Etihad mwezi huu Juni 2022 baada ya kuhudumu ugani Etihad kwa kipindi cha miaka tisa.

Phillips, 26, amechezea Leeds mara 214 tangu aanze kuvalia jezi za kikosi cha kwanza mnamo 2015.

Sasa anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Jude Bellingham, Jordan Henderson, Conor Gallagher na James Ward-Prowse ili kuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na Uingereza katika fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Arsenal kusajili Gabriel Jesus wa Man-City ili kuziba pengo...

FIFA yaidhinisha vikosi vya masogora 26 kwa ajili ya Kombe...

T L