Man-United wajiondoa katika mbio za kumsajili fowadi Marko Arnautovic

Man-United wajiondoa katika mbio za kumsajili fowadi Marko Arnautovic

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United wamejiondoa katika mbio za kuwania maarifa ya mvamizi Marko Arnautovic kutoka kambini mwa Bologna.

Kocha mpya wa Man-United, Erik ten Hag, amekuwa akifukuzia huduma za Arnautovic – nyota mzoefu raia wa Austria aliyewahi kunolewa na mkufunzi huyo raia wa Uholanzi kambini mwa FC Twente.

Hata hivyo, Man-United wametamatisha azma ya kumsajili Arnautovic baada ya Bologna kudai kiasi kikubwa fedha kwa ajili ya fowadi huyo.

Man-United walifichua mpango wa kumsajili Arnautovic baada ya Brighton kuwapepeta 2-1 katika mchuano wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu wa 2022-23 mnamo Agosti 7, 2022 ugani Old Trafford.

Arnautovic aliwahi kufunga mabao 43 kutokana na mechi 184 akichezea West Ham United na Stoke City kati ya 2013 na 2019.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Wakenya wadumishe amani wakisubiri matokeo ya...

Kieni: Kanini Kega akubali sauti ya wapigakura akae kando

T L