Maneja wa Bandari asifu kikosi chake kwa kuzima Ulinzi

Maneja wa Bandari asifu kikosi chake kwa kuzima Ulinzi

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MENEJA wa Bandari FC, Albert Ogari aliwasifu wachezaji wa timu yake kwa kufanikiwa kurudi safari yao ya Kericho wakiwa na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ulinzi Stars FC kwenye mechi ya Ligi Kuu ya FKF.

Ogari alisema wachezaji wao waliopewa jukumu la kucheza mchezo huo, walicheza kwa kujitolea na ari ya kuhakikisha wanatoka uwanjani na ushindi.

“Ninawajibu wa kuwasifu wanasoka wetu na kuwapa shukrani nyingi kwa kucheza mchezo huo kwa njia iliyoifanya timu yetu ikiibuka washindi kutokana na mabao mawili yaliyofungwa na Benjamin Mosh na Darius Msagha,” akasema meneja huyo.

Anasema wachezaji wanatarajia kurudi uwanjani kuandaliwa na kocha Andreb Casa Mbungo kwa ajili ya kujitayarisha kwa mechi yao nyingine ya ligi hiyo dhidi ya Nzoia Sugar itakayopepetwa uwanja wao wa nyuymbani wa Mbaraki Sports Club siku ya Jumamosi hii.

“Tunazihitaji pointi hizo tatu tutakapokutana na Nzoia na hivyo, wanasoka wataongeza bidi katika mazoezi ili tuzidi kupanda ngazi na kuwa mojawapo ya timu zenye kutegemea kushinda ligi ya msimu huu,” akasema Ogari.

Baada ya mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa Kericho, Bandari imeruka hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali la ligi hiyo ikiwa na pointi 25 baada ya mechi 14, ikipitwa na Tusker iliyo kileleni kwa alama saba huku ikipitwa kwa pointi moja pekee na KCB iliyoko nafasi ya pili.

Lakini timu iliyoko chini ya Bandari ambayo ni AFC Leopards pia iko na pointi 25 lakini imecheza mechi 12, hivyo timu ya Pwani inahitajika ihakikishe inashinda mechi zao na kuiombea Leopards wapoteze wabakie kwenye nafasi hiyo ya tatu.

You can share this post!

MMvita Youngstars yailima Annex 07 FC 3-0

Mimi si mchawi – Raila Odinga