• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 11:20 AM
CECIL ODONGO: Jamii ya kimataifa iingilie kati na kufanya patanisho ya Rais Ruto, Raila

CECIL ODONGO: Jamii ya kimataifa iingilie kati na kufanya patanisho ya Rais Ruto, Raila

Vigogo hao wawili wanahitaji patanisho la kisiasa, tena haraka kabla maji yazidi unga.Jumatatu iliyopita, Bw Odinga alitoa kauli kwamba hatambui utawala wa Rais Ruto baada ya ripoti ya mfichuzi kuanika jinsi Waziri Mkuu huyo wa zamani ndiye alishinda uchaguzi wa urais.

Bw Odinga akaweka wazi kuwa anapanga msururu wa maasi dhidi ya serikali ya Ruto.

Huenda maandamano hayo yashike kasi ikizingatiwa Wakenya wengi wamelemewa na gharama ya juu ya maisha na wanapinga mpango wa serikali kuwaongezea ushuru.

Hata baadhi ya wafuasi wa Kenya Kwanza wamelalamika mitandaoni kwamba serikali haifanyi chochote kubadili maisha haya magumu, na badala yake wamejikita kumshambulia Bw Odinga mara kwa mara.

Rais naye pia amesisitiza hatetereki kwa maandamano ya Bw Odinga, akisema ni ya kumshinikiza akubali waridhiane ndipo ammege sehemu ya utawala wake.

Ikiwa misimamo na cheche kali kati ya vigogo hao wa siasa zitaendelea, basi ni wazi nchi haitapiga hatua zozote kimaendeleo.

Kenya ni kati ya nchi zinazotegemewa na majirani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na pia Afrika nzima.

Iwapo kutakuwa na misukosuko kutokana na uhasama kati ya Rais na Bw Odinga, basi itakuwa siasa na cheche kwa miaka mitano.

Wawekezaji watatoroka sababu ya mazingira yasiyoridhisha kibiashara.

Viongozi wa kimataifa wasisubiri kuanza juhudi za upatanishi wakati nchi imetumbukia, bali walete patanisho sasa hivi kati ya serikali na upinzani.

Vigogo wakiendelea kushikilia misimamo mikali taifa litaendelea kuwa mateka, gharama ya maisha itazidi kupanda na mwananchi wa kawaida atabaki kuumia hata zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Wanaraga Kabras Sugar tayari kuchezesha densi...

KASHESHE: Elba aipa shavu KE

T L