• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
LEONARD ONYANGO: Itabidi Mudavadi akubali wadhifa wa uwaziri serikali ijayo 2022

LEONARD ONYANGO: Itabidi Mudavadi akubali wadhifa wa uwaziri serikali ijayo 2022

Na LEONARD ONYANGO

KIONGOZI wa Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi, ni miongoni mwa wanasiasa wanaokabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha wanafanya maamuzi yatakayowasaidia kuwa serikalini baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Kura za maoni za hivi punde zinaonyesha kuwa, ni asilimia moja tu ya wapiga kura watachagua Bw Mudavadi ikiwa uchaguzi huo utaandaliwa leo. Hiyo inamaanisha kwamba, uwezekano wa Bw Mudavadi kushinda urais 2022 ni sawa na farasi kupita katika tundu la sindano. Bw Mudavadi anastahili kufanya mambo matatu: aunge mkono Naibu wa Rais William Ruto au kinara wa ODM Raila Odinga au awanie urais kupitia muungano wa One Kenya Alliance (OKA).

Akiunga mkono Bw Ruto au Bw Odinga, uwezekano wake wa kuwa mwaniaji mwenza ni mfinyu mno. Dkt Ruto na Bw Odinga tayari wameonyesha nia ya kuteua wawaniaji wenza kutoka eneo la Mlima Kenya. Iwapo Bw Mudavadi ataamua kuunga mkono Bw Odinga au Dkt Ruto, itabidi ajiandae kutwaa wadhifa wa uwaziri au ubalozi.

Katiba hairuhusu Dkt Ruto kuwa Naibu wa Rais kwa muhula wa tatu – hivyo hana jingine bali kuwania urais.

Kwa kuungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta na mabwanyenye kutoka eneo la Mlima Kenya, Bw Odinga anaamini uchaguzi wa Agosti 9 utamfungulia njia ya kuingia Ikulu.

Itakuwa vigumu kwa Bw Odinga kuunga mkono mwaniaji mwingine kwani wandani wake wanaamini tayari ameanza ‘kunusia’ hewa ya Ikulu. Bw Mudavadi akiamua kusimama kidete na kuwania urais kupitia tiketi ya OKA, itakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha vinara wenzake wa muungano huo hawamtoroki kabla ya Agosti 9, 2022.

  • Tags

You can share this post!

UJASIRIAMALI: Wadudu kama nzi hivi, kwake dhahabu

Man-Utd wakataa ofa kutoka kwa Sevilla ya kumtwaa Martial...

T L