• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 11:46 AM
MITAMBO: Mtambo safi katika uundaji lishe toka makapi ya mahindi

MITAMBO: Mtambo safi katika uundaji lishe toka makapi ya mahindi

NA PETER CHANGTOEK

WAKULIMA wa mahindi kutoka maeneo tajiri ya Uasin-Gishu, Nandi na Trans-Nzoia kwa siku nyingi wamekuwa wakipinga hatua ya serikali kuagiza mahindi kutoka nchi jirani.

Aidha, baadhi wamekuwa wakishinikiza serikali kuongeza bei ya gunia la kilo 90 la mahindi, ikizingatiwa kuwa wakulima wengi wao sasa hivi wanauza mahindi kwa Sh4,500.

Geoffrey Tenai kutoka eneo la Moiben, Kaunti ya Uasin-Gishu anasema matatizo ya wakulima kwa upande mmoja husababishwa na mabroka ambao hununua bidhaa kwa bei duni na kuyauza kwa bei ghali.

Pili, visa vya mabadiliko ya tabianchi kwa mfano kupungua kwa kiwango cha mvua nchini na uhaba wa maji, ndio chanzo cha mavuno kudorora.

“Bila kusahau ukosefu wa soko la uhakika umekuwa ukisababisha upotevu wa mazao hususan baada ya kuvuna, wakati ambao mahindi huwa yamefurika sokoni,” akasema.

Kulingana na Tenai, kwa wakati mmoja mwaka wa 2021, bei ya kilo 90 ya gunia la mahindi ilikuwa imeshuka hadi Sh2500, jambo ambalo lilimvunja moyo kibinafsi akiwa mpanzi wa mahindi katika kipande cha ardhi cha ekari tano.

Hata hivyo, baadhi ya wakulima ambao wamekuwa wakikuza mahindi kwa muda mrefu wamebuni njia mbadala ya kutumia makapi au punje za mahindi kujikwamua kiuchumi kwa kutengeneza malisho.

Ikumbukwe kuwa gharama ya pembejeo, mbolea, nguvu kazi, uvunaji, kupakia na kusafirisha mazao sokoni huwa ni kubwa ikilinganishwa na faida ambayo mkulima hutengeneza kutoka kwenye gunia moja.

Geoffrey Gitonga kutoka eneo la Kiamunyeki Nakuru anasema amekuwa akikuza mahindi kutengeneza lishe ya kulisha mifugo wake.

Gitonga anasema kuwa kukuza malisho kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ni nafuu, ikilinganishwa na hatua ya wakulima wengi wa mifugo kutegemea malisho kutoka viwandani.

Akilimali ilipomtembelea nyumbani kwake, tulimkuta akipakia silage ambayo imetengenezwa na makapi ya mahindi kisha kusafirishwa katika maeneo mengine ya Dundori, Freearea na Bahati kwa wakulima wengine ambao hufuga ng’ombe wa maziwa.

Kwa Gitonga, hii imetoa fursa ya ajira hususan msimu huu wa kiangazi kirefu wakati ambao upatikanaji wa lishe za mifugo ni nadra , na vilevile anaweza kuwalisha mifugo wake bila changamoto.

Anasema hii ni njia mojawapo ya kuboresha masalio ya shambani na njia rahisi kwa wakulima wadogo kumudu gharama ya ufugaji.

Wafanyakazi katika Kiamunyeki Sams Farm, Nakuru wakipakia malisho ambayo yameundwa kutokana na makapi ya mahindi. Utengenezaji lishe kutokana na makapi haya huokoa wafugaji wakati wa kiangazi. PICHA | RICHARD MAOSI

Anaongezea kuwa kwa kipindi cha miezi sita hivi iliyopita maeneo ya Naivasha, Lanet, Laikipia, Baringo na Njoro hayajakuwa yakipokea mvua wa kutosha jambo ambalo limewasukuma wakulima kujitafutia malisho katika maeneo jirani na hatimaye kusababisha mtafaruko baina ya binadamu na mifugo.

Anasema hutumia sehemu kubwa ya shamba lake kuyakuza mahindi ambayo hutumika kama lishe, ambapo mara tu baada ya kuvuna mahindi huyakata vipande vipande kwa kutumia aina maalum ya mtambo.

Kisha huyachanganya na molasses, kisha huwekwa ndani ya mfuko mkubwa au kufunikwa kwenye ardhi tambarare na kuhakikisha kuwa hewa haipenyi.

“Katika kipindi cha baina ya miezi 3-4 silage ya mkulima huwa tayari na inaweza kutumika msimu wa kiangazi,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

ZARAA: Aliachana na mahindi kahawa iliponyanyuka

Mkutano ulituletea ushindi, adai Kane

T L