• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
TAHARIRI: Mchango wa Ingwe ni muhimu katika soka

TAHARIRI: Mchango wa Ingwe ni muhimu katika soka

NA MHARIRI

SHIRIKISHO la Soka Nchini (FKF) limejifunza mengi siku chache tu baada ya kuwapiga marufuku mashabiki wa klabu ya AFC Leopards.

Leopards ndiyo klabu yenye mashabiki wengi nchini kwa sasa lakini tangu wazimwe kuenda viwanjani kushangilia timu yao mechi zinazohusu timu hiyo, zimekuwa hazina mvuto wowote.

Ligi kuu ina timu 18, lakini inavyoonekana, hakuna timu nyingine iliyo na mashabiki kama Ingwe ambao wamekuwa wakitumia mabasi kusafirisha mashabiki wao kwenda viwanjani kutazama mechi.

Lakini tangu waamrishwe kukaa nyumbani, timu nyingine 17 zimeshindwa kuvutia hata mashabiki 300, hii ikidhihirisha jinsi klabu hiyo ilivyo na wafuasi wengi.

Kila timu imekuwa ikingojea kwa hamu kukutana na Leopards ili angalau ijipatie hela wakati huu mgumu kiuchumi.

Bila Leopards katika ligi kuu, mpira wa Kenya umeonekana kukosa ladha, lakini ni miongoni mwa timu ambazo zimekuwa zikionewa mara kwa mara na FKF.

Kuna wakati klabu hii ilipigwa faini ya Sh6 milioni kwa kukataa kwenda Thika kucheza mechi ya Debi dhidi ya Gor Mahia, wakati Gor wakipigwa faini ya Sh3 muhimu wa klabu hiyo kwenye soka ya Kenya umeilazimu FKF kuruhusu mashabiki wa klabu hiyo kurejea uwanjani kuanzia wikendi hii.

Barua iliyowekwa saini na Afisa Mkuu wa FKF, Barry Otieno ilisema kamati ya kusikiza kesi za rufaa katika shirikisho hilo ilikutana Alhamisi na kuamua marufuku ya mechi iliyowekewa mashabiki wa klabu hiyo iondolewe ili waanze kurudi uwanjani kushangilia timu yao ambayo kesho Jumapili itakabiliana na Nzoia Sugar FC, ugani Nyayo.

Chini ya mwenyekiti Janet Katisya, kamati hiyo ilisema imesikiza kesi ya kujitetea kutoka kwa klabu hiyo na kuamua kulegeza kamba.Mashabiki wa Leoparda walipigwa marufuku kuingia uwanjani baada ya kuhusishwa na fujo zilizotokea uwanjani Bukhungu mnamo Aprili 19 ambapo mwamuzi wa mechi alijeruhiwa. Mbali na kupigwa marufuku na kupokonywa pointi tatu, klabu hiyo vile vile ilitozwa Sh500,000 kufuatia fujo hizo zilizotokea wakicheza na Kakamega Homeboyz kabla ya mechi hiyo kutibuka dakika 34 Homeboyza wakiongoza kwa 1-0.

Leopards pia iliamrishwa igharamie malipo ya hospitali ya refa Micheal Obuya aliyeumia siku hiyo, lakini usimamizi wa klabu hiyo uliamua kufuata utaratibu kuhakikisha haki imetendeka kwa ajili ya kudumisha heshima ya timu hiyo kongwe.FKF kadhalika ilipendekeza kocha mkuu wa klabu hiyo, Patrick Aussems na naibu wake Lawrence Webo wafanyiwe uchunguzi baada ya kuvuruga amani siku hiyo.

Tangu ipigwe marufuku, mashabiki wa Leopards wamekuwa wakilipa ada za kuingia uwanjani hata wakiwa nyumbani ili kusaidia timu hiyo moja kwa moja, na kukataa kabisa kusafiri kuchangia timu pinzani.

Akizungmza kuhusu hatua ya FKF, mwenyekiti wa klabu hiyo, Dan Shikanda alisema timu yake imekuwa ikidhulumiwa bila hatua kuchukuliwa.

Alisema kutibuka kwa mechi mjini Kakamega kulitokana na uzembe wa mwamuzi na ukosefu wa askari wa kutosha siku hiyo.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Uhusiano wa Urusi na Afrika utawaramba...

NYOTA WA WIKI: Callum Wilson

T L