• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
TAHARIRI: SJAK iwe mfano bora kuongoza uchaguzi huru, wa uwazi na haki

TAHARIRI: SJAK iwe mfano bora kuongoza uchaguzi huru, wa uwazi na haki

NA MHARIRI

MUUNGANO wa Wanahabari wa Michezo nchini (SJAK), umepanga kufanya uchaguzi wake Machi 4, 2023 ambapo maafisa wapya watateuliwa kuchukua nafasi ya wale wa zamani ambao wametawala kwa miaka minne.

SJAK ilizinduliwa mwaka wa 2014 ikiwa na malengo kadhaa. Mojawapo ikiwa ni kuboresha michezo nchini kwa kuchukua jukumu kuu katika kuhamasisha udugu wa michezo na pia kuwatuza wanamichezo bora kila mwezi.

Mara ya mwisho uchaguzi huo uliandaliwa ilikuwa mwaka 2018 ambapo maafisa wafuatao walichaguliwa; Chris Mbaisi (Rais), James Magayi (Makamu wa Rais), Mike Okinyi (Katibu Mkuu), Wanjiku Mwenda (Mweka Hazina). Alex Isaboke, Michelle Katami, Samson Ateka, Vereso Mwanga na Evelyn Watta (Wajumbe wa Kamati).

Kufikia sasa, kuna sintofahamu kuhusu orodha ya wawaniaji na viti ambavyo viko wazi kuwaniwa.

Mwaka 2018, SJAK kupitia katibu mkuu wake walidai kwamba, kamati teule (Executive) ilikuwa na mamlaka kisheria kuamua kuteua watakaosalia mamlakani bila kuhusisha wanachama wao.

Kufuatia hilo, malalamishi yameibuliwa na kundi la wanahabari linalojiita Nguvu Mpya ambalo baadhi ya wanachama wake wananuia kupigania viti kwenye uchaguzi huo.

Katika kujibu kwa haraka, Katibu Mkuu wa SJAK anayeondoka Mike Okinyi alisema kundi hilo ambalo linataka kuingia mamlakani linafaa kuwavutia wapiga kura na kuacha woga.

Muda wa mwisho wa uteuzi ulifungwa jana Ijumaa.

“Team Nguvu Mpya” inasema hakuna hoja zozote zilizoibuliwa kwa viongozi wa muungano huo zimeshughulikiwa licha ya kuiandikia barua ofisi ya sasa mara kadhaa.

Kundi hilo la Nguvu mpya linaongozwa na James Waindi, ambaye ni Mhariri wa Michezo katika gazeti la People Daily, Moses Wakhisi (Katibu mkuu wa Standard Group), Eric Njiru (Homeboyz Radio, Makamu wa Rais), Mukami Wambora (katibu mratibu), Cellestine Olilo (mweka hazina NMG), na wanachama Abula Ahmed (K24), Agnes Makhandia (NMG), Geoffrey Mwamburi (Radio Citizen), Dennis Okeyo (Standard Group) na Charity Wanja.

Kundi hilo linadai kuwa lengo lake ni kuwafamisha wanachama kinachoendelea tunapoendelea baada ya uongozi wa SJAK kuwa kimya wakati uchaguzi unazidi kukaribia.

Kutokana na vuta nikuvute baina ya viongozi wa zamani na wanachama, SJAK iko hatarini kujiabisha kiasi cha kutoweza kujisafisha hapo baadaye.

Ni lazima kundi hili lidhihirishe hadhi wanahabari wanapewa nchini na ulimwenguni kote kwa kuwa kilelezo bora katika uandaaji uchaguzi huru, uliojaa uwazi na wa haki wiki ijayo.

Endapo vigezo hivyo vitakosekana basi haitakuwa muhali wanahabari kuwa msitari mbele kutetea haki katika jamii kwa ujumla

  • Tags

You can share this post!

Samburu walilia usalama majangili wakiendeleza mashambulio

Wito mradi wa gesi wa Taifa uwafaidi wakazi wa Pwani

T L