• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
WANDERI KAMAU: Hatua zichukuliwe kuwaokoa Wakenya wanaotesekea nchi za Uarabuni

WANDERI KAMAU: Hatua zichukuliwe kuwaokoa Wakenya wanaotesekea nchi za Uarabuni

NA WANDERI KAMAU

SIMULIZI za Wakenya wanaokumbana na mateso katika nchi za Arabuni ni za kuatua moyo.

Binafsi, nimechoshwa na simulizi hizi za kuogofya.

Naam, nimechoka kuwasikia akina dada wetu wakieleza madhila, mahangaiko na hujuma wanazokumbana nazo katika nchi za Ghuba.

Nimeacha hata kutazama video wanazotuma kutoka katika nchi hizo, kwani huwa najikuta nikibubujikwa na machozi.

Mara nyingine, huwa nashindwa hata kufanya kazi zangu binafsi ninapowaza kuhusu hali wanazojikuta akina dada hao.

Hata hivyo, hali hii imedumu kwa muda mrefu.

Ni miaka na mikaka sasa tangu nilipoanza kusikia malalamishi ya wanawake wanaoenda kufanya kazi katika mataifa hayo.

Swali langu ni: Hali hii itatatuliwa vipi? Wahusika wakuu wako wapi? Huwa wanachukua hatua zozote? Huwa wanatazama au kufikiwa na vilio hivyo

Ni taswira za kusikitisha wakati familia zinaagana na jamaa zao wakiwa hai wanapoelekea huko na baadaye kurejea wakiwa maiti.

Kulingana na tamaduni za Kiafrika, si vizuri wakati mzazi anapomzika mwanawe.

Hata hivyo, hali ndivyo imekuwa kwa vijana barobaro wanaoenda Arabuni, kwani baadhi yao wamerejeshwa makwao wakiwa kwenye majeneza—wasijue wala kufahamu yanayoendelea.

Sikitiko jingine ni kuwa familia nyingi huwa zinafahamishwa kuhusu vifo vya jamaa zao wiki kadhaa au hata baada ya miezi tangu wakati wanapofariki.

Pengine hakuna huzuni kubwa kuliko kama hiyo katika maisha tuishiyo hapa duniani.

Katika mvurugiko huu wote wa matukio, ni nani anapaswa kulaumiwa?

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Wakenya waliofungwa jela Uganda hawafai...

Huduma ya simu kusaidia kudhibiti maradhi yasiyoambukizwa

T L