• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:55 PM
WANDERI KAMAU: Kwa kuwatoza ‘mama-mboga na boda’ ada mpya, Ruto amewasaliti mahasla

WANDERI KAMAU: Kwa kuwatoza ‘mama-mboga na boda’ ada mpya, Ruto amewasaliti mahasla

NA WANDERI KAMAU

RAIS William Ruto alichaguliwa na Wakenya wengi kwa ahadi ya kuwatetea watu wa kiwango cha chini, yaani mahasla.

Ahadi hiyo ndiyo iliyowafanya Wakenya wengi wa tabaka la chini kumpigia kura kwa wingi, kwani walimwona kama ‘Musa’ ambaye hatimaye angeowaokoa kutoka katika changamoto nyingi za kiuchumi zilizowakabili.

Sababu nyingine iliyowapa raia msukumo wa kumchagua ni kuwa Rais Ruto amekuwa akijisawiri kama mmoja wa Wakenya hao—amekuwa akisema “alianzia chini” kwa kazi ya kuuza kuku.
Katika hali hiyo, Wakenya wengi walishawishika kuwa Dkt Ruto ndiye kiongozi aliyefaa kuiongoza nchi katika safari ya kujiokoa kiuchumi.

Hata hivyo, inasikitisha kuwa baada ya miezi sita akiwa uongozini, Rais Ruto na utawala wake wanaonekana kusahau ahadi walizowapa Wakenya. Kwa mfano, Halmashauri ya Kukagua Ubora wa Bidhaa Kenya (KEBS) imesema kuwa itaanza kuwatoza wafanyabiashara wadogo wadogo ada maalum ya Sh1,000 kwenda juu kila mwezi.

Ada hiyo inafanana na ushuru, ijapokuwa serikali imesema itakuwa ikitozwa na KEBS badala ya Halmashauri ya Kukusanya Ushuru Kenya (KRA).

Kinachoshangaza ni kuwa katika mpango huo, serikali inawalenga wafanyabiashara wadogo wadogo, iliyokuwa imeapa kuwalinda na kuwatetea kwa kila hali.
Bila shaka, huu ni usaliti mkubwa kutoka kwa serikali dhidi ya Wakenya ambao iliapa kuwalinda. Ijapokuwa lengo la Rais Ruto ni kupunguza kiwango cha mikopo inayokopa kutoka nchi za nje, huu ni mkakati utakaoipotezea uungwaji mkono kutoka kwa raia.

  • Tags

You can share this post!

Angika daluga za ulingo wa kisiasa, Kidero amwambia Raila

Kisanga kituo cha polisi Nakuru wanaume 2 wakihubiri juu ya...

T L