• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
WANDERI KAMAU: Ni ukiukaji mkubwa wa katiba kudhalilisha walemavu, wasiojiweza

WANDERI KAMAU: Ni ukiukaji mkubwa wa katiba kudhalilisha walemavu, wasiojiweza

WALEMAVU ni miongoni mwa makundi yaliyotengwa katika jamii—sawa na vijana, wanawake na jamii zinazoishi katika maeneo kame.Ili kuimarisha uwakilishi wao katika ulingo wa siasa, kumekuwa na kila juhudi kuhakikisha makundi hayo yamepata nafasi sawa za uwakilishi na wanajamii wengine.

Ni makundi yaliyolindwa vikali na Katiba, ambapo yeyote anayepatikana akiyaingilia huwa anakabiliwa vikali kisheria.Hata hivyo, inasikitisha wakati jamii inaingiza mzaha na kuwatania watu hao kwa misingi ya udhaifu wao.Ni tukio lililoshuhudiwa Jumatano katika Bunge la Kitaifa, wakati mbunge Babu Owino (Embakasi Mashariki) alificha mikongojo ya mbunge maalum David Sankok, ambayo huwa inamsaidia kutembea.

Bw Sankok ni miongoni mwa wabunge kadhaa walioteuliwa kuwaakilisha walemavu nchini katika Bunge la Kitaifa.Ingawa ni tukio lililochukuliwa kimzaha, hasa na wabunge waliokuwepo, ni wazi kuwa hilo si jambo la kuchezea hata kidogo.Kwanza, haikubainika sababu zilizochangia Bw Owino kunyakua mikongojo ya Bw Sankok, ikizingatiwa wawili hao wako katika mirengo tofauti ya kisiasa.

Bila kujali hali iliyomfanya Bw Owino kufanya hivyo, ni makosa kwa yeyote kuwatania walemavu, wanawake ama kundi lolote lililotengwa katika jamii.Ni tukio la kufadhaisha, ikiwa hii si mara ya kwanza kwa Bw Owino kuwatania au kuwatusi watu walemavu kwa sababu za kisiasa.

Miezi kadhaa iliyopita, mbunge huyo alitoa matamshi yasiyoandikika dhidi ya Seneta Maalum Isaac Mwaura, ambaye ni zeruzeru. Kama Bw Sankok, Seneta Mwaura yuko katika mrengo tofauti wa kisiasa na Bw Owino. Ni makosa wakati mtu wa hadhi ys juu kama mbunge anaingiza mzaha kwa masuala yenye uzito kama hayo.

Mbunge huyo apasa kuomba [email protected]

You can share this post!

MUTUA MUEMA: Tusherehekeni Krismasi ndio, lakini tusivuke...

Robert Lewandowski mashine ya kufunga mabao

T L