Maonyesho ya kimataifa ya vitabu yarejea baada ya kutatizwa na corona

Maonyesho ya kimataifa ya vitabu yarejea baada ya kutatizwa na corona

NA LEONARD ONYANGO

MAONYESHO ya Kimataifa ya Vitabu ambayo hufanyika kila mwaka jijini Nairobi yamerejea tena baada ya kutatizwa na janga la corona kwa miaka miwili.

Maonyesho hayo yatang’oa nanga Jumatano, Septemba 28, hadi Jumapili katika jumba la Sarit Centre jijini Nairobi.

Kulingana na mwenyekiti wa maonyesho hayo, Bi Mary Maina, wachapishaji wa vitabu 38 wa humu nchini na kimataifa watashiriki maonyesho hayo ya 23.

Mwenyekiti wa Wachapishaji Vitabu Nchini – Kenya Publishers Association- Bw Kiarie Kamau (kati), Mkurugenzi wa Bookmark Africa Lutalala Kakai (kulia) na Afisa Mkuu Mtendaji wa Longhorn Publishers Maxwell Wahome wahutubia wanahabari katika hoteli ya Sarova Stanley jijini Nairobi mnamo Jumapili, Septemba 25, 2022. PICHA | DENNIS ONSONGO

Miongoni mwa wachapishaji wa kimataifa watakaoshiriki maonyesho hayo ni Big Bad Wolf kutoka nchini Malaysia.

Maonyesho ya jijini Nairobi ambayo hutoa fursa kwa wanafunzi, walimu na wazazi fursa ya kununua vitabu vya shuleni na vinginevyo, yalikosa kufanyika 2020 na mwaka jana kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa corona.

“Mnamo 2020 maonyesho yalifanyikia mtandaoni na zaidi ya watu 100,000 walihudhuria lakini wachapishaji waliuza vitabu vichache,” akasema Bi Maina.

Jumamosi, washindi wa Tuzo za Jomo Kenyatta/Wahome Mutahi watatangazwa na kutunukiwa.

Vitabu vya Kiswahili vinavyoshinda katika kitengo cha watu wazima ni:

 1. Tubadilishe Jina chake Leonard Sanja (kimechapishwa na Oxford University Press)
 2. Kwenzi Gizani cha Kithaka wa Mberia (Marimba Publishers)
 3. Wema Waliobaki cha Alphonce Ndambuki (Oxford University Press).

Katika kitengo cha vijana, vitabu vinavyoshindana ni;

 1. Mbona Hivi cha Shullam Nzioka (Oxford University Press)
 2. Makovu ya Uhai chake Shisia Wasilwa (Queeenex Publishers)
 3. Taabu za Tabu cha Mathias Momanyi (EAEP).

Katika kitengo cha vijana, vitabu vinavyomenyana ni:

 1. Tatizo la Mamba cha Odhiambo Obura (JKF)
 2. Fumbo la Watamu cha Ali Attas (One Planet)
 3. Pala wa Zena na Hadhithi Nyingine chake Pauline Kea (Queenex Publishers).

Vitabu vya Kiingereza vinavyoshindania tuzo hizo katika kitengo cha watu wazima ni:

 1. Leading Light cha Kithusi Mulonzya
 2. The Way Vagabond cha M. G. N. Kahende
 3. The Havoc of Choice cha Wanjiru Koinange.

Katika kitengo cha vijana ni:

 1. A Journey to Becoming chake Prof Egara Kabaji
 2. Benji’s Big Win cha Nducu wa Ngugi
 3. Let’s Talk About This cha Moraa Kitaa

Katika kitengo cha watoto ni:

 1. The Secret Wish cha Jennie Marima
 2. Chadi’s Trip cha Sarah Haluwa
 3. The Yao Stories cha Seth Mboya.

Katika kitengo cha vitabu vya lugha ya ucheshi, ni vitabu viwili pekee vya Kiingereza ambavyo vinashindania tuzo ya Wahome Mutahi Prize.

Vitabu hivyo ni:

 1. Fools’ Express cha Charles Okoth
 2. Hustlers’ Chains cha Samuel Wachira
 • Tags

You can share this post!

MWALIMU: Siri yake darasani iko katika nyimbo

Wazee Mlimani waapa kuleta Kenya pamoja

T L