Habari Mseto

Mapato duni yameza kampuni tatu NSE 20 bora

April 8th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni tatu zimeondolewa katika orodha ya 20 bora katika Soko la Hisa (NSE) kwa sababu ya biashara iliyodhoofika.

Kampuni hizo ni Stanbic Holdings Plc, Sasini Limited na kampuni ya Bima ya CIC.

Nafasi ya Housing Finance Group ilichukuliwa na Nairobi Securities Exchange Plc. Kampuni tatu zilikuzwa na kuorodheshwa katika orodha ya 25 bora.

Kampuni hizo ni Kenya Reinsurance Corporation Limited, NIC Group Plc na Nairobi Securities Exchange Plc.

Katika taarifa, NSE ilielezea kuwa kuondolewa kwa kampuni hizo katika orodha hiyo kuliambatana na jinsi mambo yalivyo sokoni.

Mambo kadhaa huzingatiwa kwa kampuni ili kuorodheshwa katika nafasi ya 20 au 25 bora. Mambo hayo ni kama uwezo wa kampuni wa mtaji, hisa zilizouzwa au kununuliwa, na uwezo wake wa kuendeleza operesheni bila kuishiwa na fedha wakati wa kipindi tathmini hiyo inapofanywa.