Habari Mseto

Mapato kutoka kwa Wakenya walio ughaibuni yaongezeka

May 26th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Serikali imepokea ongezeko la mapato kutoka kwa wananchi wanaoishi nje ya nchi wakati wa robo ya mwanzo ya 2018.

Mapato hayo yaliongezeka maradufu katika kipindi hicho ikilinganishwa na 2017. Katika muda kati ya Januari na Machi, wananchi wanaoishi nje ya nchi waliwasilisha nchini Sh20.99 bilioni zaidi.

Hivyo, katika kipindi hicho, serikali iliweza kupokea Sh64.4 bilioni kutoka kwa wananchi hao.

Ukuaji huo unatokana na hali ya uchumi iliyoimarika na kuondolewa kwa adhabu na Mamlaka ya Kutoza Ushuru nchini (KRA).

Habari hii ni kwa mujibu wa mchanganuzi wa uchumi wa Stanbic Jibran Qureishi.

Mwaka wa 2017, wananchi wanaoishi nje ya nchi walituma nyumbani Sh197.12 billion, ukuaji wa asilimia 13.09 ikilinganishwa na 2016 ambapo walituma Sh174.30 bilioni.