Habari

Mapinduzi seneti

May 11th, 2020 1 min read

Na CHARLES WASONGA

HATIMAYE Rais Uhuru Kenyatta amefanikisha mapinduzi ya uongozi wa mrengo wa Jubilee katika Seneti kwa kuteua Seneta wa Pokot Magharibi Samuel Poghisio kuwa Kiongozi wa Wengi kwa kumvua Kipchumba Murkomen wadhifa huo.

Naye Seneta wa Nakuru Susan Kihika ametimuliwa kutoka wadhifa wake wa Naibu Kiranja wa Wengi na nafasi yake ikapeanwa kwa Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata. Naibu wake atakuwa Seneta Maalum Bi Haji Farhiya Ali.

Naibu wa Bw Poghisio atakuwa ni Seneta wa Isiolo Bi Fatuma Dullo ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huo chini ya uongozi wa Murkomen.